Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme wake kupitia Kanisa

Kipindi cha 6 : Wito wa Utumishi

77

d. Je, ushuhuda wangu katika Yesu Kristo ni halisi na wenye uwezo wa kuvuta wengine? Flp. 2:17

22 – Naam, hata nikimiminwa juu ya dhabihu na ibada ya imani yenu, nafurahi; tena nafurahi pamoja nanyi nyote. 18 Nanyi vivyo hivyo furahini, tena furahini pamoja nami. 19 Walakini natumaini katika Bwana Yesu kumtuma Timotheo afike kwenu karibu, nifarijiwe na mimi, nikiijua hali yenu. 20 Maana sina mtu mwingine mwenye nia moja nami, atakayeiangalia hali yenu kweli kweli. 12 Maana wote wanatafuta vyao wenyewe, sivyo vya Kristo Yesu. 22 Ila mwajua sifa yake, ya kuwa ametumika pamoja nami kwa ajili ya Injili, kama mwana na baba yake.

e. Je, ninadumisha mwenendo wenye nidhamu mbele za Mungu kupitia umahiri wangu wa nidhamu za kiroho na upendo wangu kwa kanisa miongoni mwa waamini? (1 Tim. 4:7-9).

f. Je, nina utayari kwa hali mpya na kujidhabihu kwa niaba ya wengine kwa ajili ya Kristo? (Flp. 1:18-21).

g. Je, moyo wangu uko wazi kuwajali na kuwahudumia wale walio hatarini zaidi na wanaoumizwa, bila matarajio yoyote ya hadhi, mamlaka, au faida ya kifedha? (2 Kor. 8:9).

h. Je, ni kweli niko tayari kutoa maisha yangu kwa niaba ya Bwana Yesu, na kuteseka kwa furaha kwa ajili ya watu wake, bila wazo lolote isipokuwa utunzwaji na ulinzi wao? (Mdo. 20:24).

II. Kuitikia Wito

A. Matokeo yake kwa huduma za mjini

Made with FlippingBook Digital Publishing Software