Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme wake kupitia Kanisa
76
Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme Wake Kupitia Kanisa
c. Kulinda na kuchunga kundi dhidi ya hatari na wanyama wakali, Mdo. 20:28 – Jitunzeni nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi ndani yake, mpate kulilisha kanisa lake Mungu, alilolinunua kwa damu yake mwenyewe. d. Kuchunga na kuwa vielelezo kwa kundi, 1 Pet. 5:1-4 – Nawasihi wazee walio kwenu, mimi niliye mzee, mwenzi wao, na shahidi wa mateso ya Kristo, na mshirika wa utukufu utakaofunuliwa baadaye; 2 lichungeni kundi la Mungu lililo kwenu, na kulisimamia, si kwa kulazimishwa, bali kwa hiari kama Mungu atakavyo; si kwa kutaka fedha ya aibu, bali kwa moyo. 3 Wala si kama wajifanyao mabwana juu ya mitaa yao, bali kwa kujifanya vielelezo kwa lile kundi. 4 Na Mchungaji mkuu atakapodhihirishwa, mtaipokea taji ya utukufu, ile isiyokauka.
e. Kuwaandaa watakatifu kwa ajili ya kazi ya huduma (Efe. 4:11-17).
2. Orodha ya mambo ya kuzingatia kwa wale wanaotafuta kutambua uhalisia wa mzigo wao wa ndani na hisia ya wito maalum:
a. Je, nimeokolewa - Je, nimetubu na kuamini Injili kuhusu uzima ambao Mungu hutoa kupitia damu iliyomwagwa na ufufuo wa Kristo? (1 Tim. 1:12-16).
b. Je, ninampenda Bwana na watu wa Mungu? Yn. 21:12 17 – Je, wanipenda? Lisha wana-kondoo wangu!
c. Je, nina karama za kiroho zinazoniruhusu kuongoza, kufundisha, na kuchunga, na je, ninatumia karama hizo kuwajenga watu wa Mungu? (2 Kor. 8:22).
Made with FlippingBook Digital Publishing Software