Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme wake kupitia Kanisa

Kipindi cha 6 : Wito wa Utumishi

75

1 Kor. 1:26-31 Maana, ndugu zangu, angalieni mwito wenu, ya kwamba si wengi wenye hekima ya mwilini, si wengi wenye nguvu, si wengi wenye cheo walioitwa; 27 bali Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vinyonge vya dunia na vilivyodharauliwa, naam, vitu ambavyo haviko, ili avibatilishe vile vilivyoko; 29 mwenye mwili awaye yote asije akajisifu mbele za Mungu. 30 Bali kwa yeye ninyi mmepata kuwa katika Kristo Yesu, aliyefanywa kwetu hekima itokayo kwa Mungu, na haki, na utakatifu, na ukombozi; 31 kusudi, kama ilivyoandikwa, “Yeye aonaye fahari na aone fahari juu ya Bwana.” vyenye nguvu; 28 tena Mungu alivichagua vitu

C. Mifano halisi kuelezea wito wa utumishi

1. Yesu Bwana wetu katika unyenyekevu wake wa kiungu (Flp. 2:5-11).

2. Bwana wetu katika Chumba cha Juu (Yn. 13:1-17).

3. Mtume Paulo, Mdo 20:22-24 – Basi sasa, angalieni, nashika njia kwenda Yerusalemu hali nimefungwa

rohoni, nisiyajue mambo yatakayonikuta huko; 23 isipokuwa Roho Mtakatifu mji kwa mji hunishuhudia akisema, ya kwamba vifungo na dhiki vyaningoja. 24 Lakini siyahesabu maisha yangu kuwa kitu cha thamani kwangu kama kuumaliza mwendo wangu na huduma ile niliyopokea kwa Bwana Yesu, kuishuhudia Habari Njema ya neema ya Mungu.

D. Ufahamu wa kipekee kwa viongozi wa kiroho: Je, lipi ni jukumu na wajibu hasa wa wale walioitwa kimaalum kutumikia jumuiya ya Kikristo?

1. Muhtasari kuhusu wale walioitwa kimaalum na majukumu yao

a. Kuujenga mwili wa Kristo, kwa maana ya kiidadi na katika ukomavu, Efe. 4:11-13 – Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu; 12 kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe; 13 hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo.

b. Kuilinda imani waliyokabidhiwa watakatifu mara moja tu (Yuda, Tit. 1:9; 2 Tim. 2:22).

Made with FlippingBook Digital Publishing Software