Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme wake kupitia Kanisa

8 Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme Wake Kupitia Kanisa

Kusudi kuu la somo hili ni kuchunguza kwa pamoja kile ambacho Maandiko yanafundisha juu ya vipengele na majukumu yanayohusiana na wito wa Mungu kwa Kanisa na uongozi wake. Zaidi ya hayo, tutachunguza kwa karibu inamaanisha nini mtu kutimiza wito wake maalum kwa kumwakilisha Yesu Kristo na Ufalme wake kwa heshima na uadilifu kupitia Kanisa. Kama matokeo ya kuchukua kozi hii, kila mwanafunzi anapaswa kuwa na uwezo wa: • Kunukuu, kufafanua, na kutumia kwa ufanisi maandiko teule yanayotoa muhtasari na kuelezea vipengele na majukumu yanayohusiana na wito halisi wa Mungu. • Kutofautisha kati ya dhana ya wito wa jumla na wito maalum wa Mungu kwa ajili ya uongozi katika Kanisa. • Kukariri na kuelezea asili ya wito wa Mungu unaohusiana na wokovu, utakatifu, uhuru na jumuiya. • Kutoa Maandiko na hoja za kuelezea wajibu wa pande mbili wa utumishi na mateso yanayohusiana na wito wa Mungu. • Kutoa muhtasari kuhusu hatua za kuelewa na kuthibitisha wito maalum wa Mungu. • Kujadili na kutoa ushahidi wa wito wako binafsi kwenye huduma, na kueleza kile unachoamini sasa kuwa ndio wito wa Mungu kwenye maisha yako, iwe katika Kanisa au katika jukumu fulani la uongozi katika Kanisa kama mwakilishi rasmi. • Kukariri kifungu teuliwa cha Maandiko kuhusu wito wa Mungu. Jambo la muhimu zaidi katika ufuasi na huduma ni mtu kutambua wito wake katika Yesu Kristo. Kama Bwana, yeye peke yake ndiye anayejiitia wanaume na wanawake, wavulana na wasichana kutoka kila nchi, tamaduni na koo ili watengwe kwa ajili yake na ufalme wake, ili watumike kama watumwa na wafungwa kwa ajili ya utukufu wake na kwa faida ya Injili. Mtu kutoa yote kwa Kristo ni kupokea yote yatokayo kwake wakati huo huo, na kwa wito huo, uzima wa milele. Bwana na akupe neema na masikio ya kusikia sauti yake ya ufasaha, na wito wake wa ujasiri na mwaliko kwa maisha ya ufuasi, huduma, na kumshuhudia Yeye na Ufalme wake.

~ Don Davis

Made with FlippingBook Digital Publishing Software