Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme wake kupitia Kanisa

Kipindi cha 7 : Wito wa Mateso

85

5. Uhakika wa utukufu: kushiriki thawabu ya Yesu

a. Rum. 8:16-17 – Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu; 17 na kama tu watoto, basi, tu warithi; warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo; naam, tukiteswa pamoja naye ili tupate na kutukuzwa pamoja naye. b. Yn. 12:25-26 – Yeye aipendaye nafsi yake ataiangamiza; naye aichukiaye nafsi yake katika ulimwengu huu ataisalimisha hata uzima wa milele. 26 Mtu akinitumikia, na anifuate; nami nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo. Tena mtu akinitumikia, Baba atamheshimu c. 2 Tim. 2:10-13 – Kwa ajili ya hilo nastahimili mambo yote, kwa ajili ya wateule, ili wao nao waupate wokovu ule ulio katika Kristo Yesu, pamoja na utukufu wa milele. 11 Ni neno la kuaminiwa. Kwa maana, Kama tukifa pamoja naye, tutaishi pamoja naye pia; 12 Kama tukistahimili, tutamiliki pamoja naye; Kama tukimkana yeye, yeye naye atatukana sisi; 13 Kama sisi hatuamini, yeye hudumu wa kuaminiwa. Kwa maana hawezi kujikana mwenyewe.

Wito wa kuteseka ni wito wa Mungu kwa wote waliokombolewa kushiriki mateso ya Mwanawe, Yesu Kristo, ili sisi nasi pia tuweze kushiriki katika utukufu wake.

C. Mifano halisi kuelezea wito wa mateso

1. Gideoni

a. Kupokea na kushindana na wito (Amu. 6:11-15).

b. Mashaka juu ya hekima ya wito huo (Amu. 6:36-40).

c. Kupata uthibitisho kuhusu timu (watenda kazi) sahihi (Amu. 7:2-7).

Made with FlippingBook Digital Publishing Software