Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme wake kupitia Kanisa
86
Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme Wake Kupitia Kanisa
1 Pet. 2:21-25 Kwa sababu ndio mlioitiwa; maana Kristo naye aliteswa kwa ajili yenu, akawaachia kielelezo, mfuate nyayo zake. 22 Yeye hakutenda dhambi, wala hila haikuonekana kinywani mwake. 23 Yeye alipotukanwa, hakurudisha hakuogofya; bali alijikabidhi kwake yeye ahukumuye kwa haki. 24 Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe hai kwa mambo ya haki; na kwa kupigwa kwake mliponywa. 25 Kwa maana mlikuwa mnapotea kama kondoo; lakini sasa mmemrudia Mchungaji na Mwangalizi wa roho zenu Rum. 8:16-17 Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu; 17 na kama tu watoto, basi, tu warithi; warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo; naam, tukiteswa pamoja naye ili tupate na kutukuzwa pamoja naye matukano; alipoteswa,
2. Petro, katika kifo chake, Yn. 21:18-19 – Akasema, “Amin, amin, nakuambia, Wakati ulipokuwa kijana, ulikuwa ukijifunga mwenyewe na kwenda utakako; lakini utakapokuwa mzee, utainyosha mikono yako, na mwingine atakufunga na kukuchukua usikotaka.” 19 Akasema neno hilo kwa kuonyesha ni kwa mauti gani atakayomtukuza Mungu. Naye akiisha kusema hayo akamwambia, “Nifuate”. 3. Mitume mbele ya Baraza la Sanhedrini Mdo. 5:40-42– nao walipowaita mitume, wakawapiga, wakawaamuru wasinene kwa jina lake Yesu; kisha wakawaacha waende zao. 41 Nao wakatoka katika ile baraza, wakifurahi kwa sababu wamehesabiwa kuwa wamestahili kuaibishwa kwa ajili ya Jina hilo. 42 Na kila siku, ndani ya hekalu na nyumbani mwao, hawakuacha kufundisha na kuhubiri habari njema za Yesu kwamba ni Kristo. 4. Mtume Paulo, 2 Tim. 4:6-8 – Kwa maana, mimi sasa namiminwa, na wakati wa kufariki kwangu umefika. 7 Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda; 8 baada ya hayo nimewekewa taji ya haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile; wala si mimi tu, bali na watu wote pia waliopenda kufunuliwa kwake.
D. Ufahamu wa kipekee kwa viongozi wa kiroho: Je, mateso yana nafasi gani katika maisha ya wale walioitwa kimaalum kuhudumu kwa ajili ya jumuiya ya Kikristo?
1. Viongozi wa kiroho mara nyingi huwa wa kwanza kupokea hasira na mapigo ya wale wanaompinga Kristo na Ufalme wake; Lk. 21:12-19 – Lakini, kabla hayo yote hayajatokea, watawakamata na kuwaudhi; watawapeleka mbele ya masinagogi, na kuwaua magerezani, mkipelekwa mbele ya wafalme na maliwali kwa ajili ya jina langu. 13 Na hayo yatakuwa ushuhuda kwenu. 14 Basi, kusudieni mioyoni mwenu, kutofikiri fikiri kwanza mtakavyojibu; 15 kwa sababu mimi nitawapa kinywa na hekima ambayo watesi wenu wote hawataweza kushindana nayo wala kuipinga. 16 Nanyi
Made with FlippingBook Digital Publishing Software