Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme wake kupitia Kanisa

Kipindi cha 7 : Wito wa Mateso

87

mtasalitiwa na wazazi wenu, na ndugu zenu, na jamaa zenu, na rafiki zenu, nao watawafisha baadhi yenu. 17 Nanyi mtachukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu. 18 Walakini hautapotea hata unywele mmoja wa vichwa vyenu. 19 Nanyi kwa subira yenu mtaziponya nafsi zenu. 2. Mateso na upinzani ni mambo yasiyoepukika kwa wale ambao ni wa Yesu Kristo na wawakilishi wa maslahi yake, Yn. 15:20 – Likumbukeni lile neno nililowaambia, “Mtumwa si mkubwa kuliko bwana wake.” Ikiwa waliniudhi mimi, watawaudhi ninyi; ikiwa walilishika neno langu watalishika na lenu 3. Unyenyekevu imara na usiohitaji sababu ni namna ambayo (kwa pamoja na Damu ya Kristo) tunazishinda nguvu za adui, Ufu. 12:10-11 – Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, “Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku. 11 Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa.” 4. Masumbufu, uchovu, na shida mara nyingi hufuatana na wale wanaomtumikia Yesu na Injili yake ; Mk. 10:29 31 – Yesu akasema, “Amin, nawaambieni, Hakuna mtu aliyeacha nyumba, au ndugu waume, au ndugu wake, au mama, au baba, au watoto, au mashamba, kwa ajili yangu, na kwa ajili ya Injili, 30 ila atapewa mara mia sasa wakati huu, nyumba, na ndugu waume, na ndugu wake, na mama, na watoto, na mashamba, pamoja na udhia; na katika ulimwengu ujao uzima wa milele. 31 Lakini wengi walio wa kwanza watakuwa wa mwisho; na wa mwisho watakuwa wa kwanza.”

2 Tim. 3:10-13 Bali wewe umeyafuata mafundisho yangu, na mwenendo wangu, na makusudi yangu, na imani, na uvumilivu, 11 na upendo, na saburi; tena na adha zangu na mateso, mambo yaliyonipata katika Antiokia, katika Ikonio, na katika Listra, kila namna ya adha niliyoistahimili, naye Bwana aliniokoa katika hayo yote. 12 Naam, na wote wapendao kuishi maisha ya utauwa katika Kristo Yesu wataudhiwa. 13 lakini watu wabaya na wadanganyaji wataendelea, na kuzidi kuwa waovu, wakidanganya na kudanganyika.

5. Ushuhuda na urithi wa watumishi wa Mungu hufunua utayari wa kupokea chochote kinachohitajika ili kutimiza huduma ya Bwana.

Made with FlippingBook Digital Publishing Software