Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme wake kupitia Kanisa
Kipindi cha 7 : Wito wa Mateso
89
(2) Kol. 1:24 – Sasa nayafurahia mateso niliyo nayo kwa ajili yenu; tena nayatimiliza katika mwili wangu yale yaliyopungua ya mateso ya Kristo, kwa ajili ya mwili wake, yaani, kanisa lake;
6. Lazima tuwe tayari kila wakati kuyatoa maisha yetu kwa ajili ya kaka na dada zetu katika Kanisa la Yesu Kristo, 1 Yoh. 3:16 – Katika hili tumelifahamu pendo, kwa kuwa yeye aliutoa uhai wake kwa ajili yetu; imetupasa na sisi kuutoa uhai wetu kwa ajili ya hao ndugu.
II. Kuuitikia Wito
A. Matokeo yake kwa huduma ya mjini
1. Kiini cha huduma zote za Kikristo ni kuyafanania maisha na huduma ya Yesu Kristo. Yeye ndiye mfano na kielelezo cha huduma zote.
2. Kwa kufuata mfano wa Yesu, uongozi halisi wa Kikristo bila shaka utahusisha kujidhabihu na kuteseka . Hakuwezi kuwa na udhuru wala mbadala kwa kanuni hii.
3. Wale wanaoongoza bila shaka wataonja mateso pamoja na wanafunzi wengine, lakini pengine wataitwa kuwakilisha maslahi ya Yesu kwa kina zaidi. Hatupaswi
kushangaa kuona viongozi wa watu wa Mungu wakikabili mateso, mapambano, na fadhaa zaidi.
4. Uvumilivu na ustahimilivu ni sifa muhimu katika kutimiza huduma ya Mungu katika mazingira magumu na kame (kama ilivyo kwa miji yetu mingi).
5. Kumtumikia Yesu na watu wake kunaweza kukugharimu kila kitu, hata uhai wako.
Made with FlippingBook Digital Publishing Software