Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme wake kupitia Kanisa
90
Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme Wake Kupitia Kanisa
6. Kuteseka kwa ajili ya Kristo ni namna mojawapo ya heshima kuu iliyotolewa kwa wale walioitwa kutumikia maslahi yake miongoni mwa watu wake.
B. Kuhusianisha somo na maisha yako leo
1. Je, nimehesabu gharama ya kuitikia wito wa Yesu juu ya maisha yangu kama mfuasi wake? Niko tayari kupokea na kustahimili chochote ambacho uamuzi kama huo unaweza kumaanisha maishani mwangu?
2. Ni nini hasa kinachoendelea kunifadhaisha au kunizuia kuhusu wazo la kumpa Bwana Yesu maisha yangu yote siku baada ya siku?
3. Je, nina hisia zozote za mashaka au kutostahili kuhusiana na suala la kuwa na uhakika kama Mungu ameniita kwake au la – kama mtoto wake? Kama kiongozi wa watu wake?
Sala na Ukiri kwa Mungu
Kwa sababu ndio mlioitiwa; maana Kristo naye aliteswa kwa ajili yenu, akawaachia kielelezo, mfuate nyayo zake. Yeye hakutenda dhambi, wala hila haikuonekana kinywani mwake. Yeye alipotukanwa, hakurudisha matukano; alipoteswa, hakuogofya; bali alijikabidhi kwake yeye ahukumuye kwa haki. Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe hai kwa mambo ya haki; na kwa kupigwa kwake mliponywa. Kwa maana mlikuwa mnapotea kama kondoo; lakini sasa mmemrudia Mchungaji na Mwangalizi wa roho zenu.
~ 1 Petro 2:21-25
Made with FlippingBook Digital Publishing Software