Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme wake kupitia Kanisa
Kipindi cha 7 : Wito wa Mateso
91
Bango Langu Liko Wazi
Mimi ni sehemu ya Ushirika wa Wasio na aibu. Nimevuka mstari. Uamuzi umefanywa. Mimi ni mfuasi wa Yesu Kristo. Sitatazama nyuma, sitaacha, sitapunguza mwendo, sirudi nyuma, au kunyamaza. Mambo yangu yaliyopita yamekombolewa; maisha yangu ya baadaye yamehakikishwa. Nimemalizana na kuishi maisha duni, mipango midogo, magoti laini, ndoto zisizo na rangi, maono yaliyofugwa, mazungumzo ya kawaida, maisha rahisi, na malengo duni. Sihitaji tena ukuu, ustawi, cheo, kuinuliwa, ​sifa au umaarufu. Si lazima niwe sahihi, wa kwanza, aliyejuu, mwenye kutambuliwa, kusifiwa, kuzingatiwa au kutuzwa. Sasa ninaishi kwa imani, nikiutegemea uwepo wake, nikienenda kwa saburi, nikiinuliwa kwa maombi, na kufanya kazi kwa nguvu. Uso wangu umekaza, mwendo wangu ni wa haraka, lengo langu ni mbinguni, njia yangu ni nyembamba, njia yangu ni mbaya, wenzangu ni wachache, Kiongozi wangu ni wa kuaminika na utume wangu uko wazi. Siwezi kununuliwa, kudanganywa, au kucheleweshwa. Sitatetereka mbele ya hitaji la kujidhabihu, wala kusita mbele ya adui, kujadili kwenye meza ya adui, au kuzunguka zunguka katika mtego wa uduni na ukawaida. Sitakata tamaa, sitanyamaza, wala kuacha mpaka nikeshe, niwekeze, niombe, nilipe gharama na kuhubiri kwa ajili ya Kristo. Mimi ni mwanafunzi wa Yesu. Lazima niendelee mpaka atakapokuja, nitoe mpaka nianguke, nihubiri mpaka wote wajue, na nifanye kazi mpaka anizuie. Na atakapowajia walio wake, hatapata shida kunitambua. . . bango langu liko wazi!
~ Tamko la Utii la kusisimua la mchungaji kijana Mwafrika kutoka Zimbabwe
Made with FlippingBook Digital Publishing Software