Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme wake kupitia Kanisa
98
Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme Wake Kupitia Kanisa
Kiambatisho cha 2 Imani ya Nikea
Na Msaada wa Kibiblia The Urban Ministry Institute
Tunaamini katika Mungu mmoja, (Kum. 6:4-5; Mk. 12:29; 1 Kor. 8:6) Baba Mwenyezi, (Mwa. 17:1; Dan. 4:35; Mt. 6:9; Efe. 4:6; Ufu. 1:8) Muumba wa mbingu na nchi (Mwa. 1:1; Isa. 40:28; Ufu. 10:6) na vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana. ( Zab. 148; Rum. 11:36; Ufu. 4:11 ) Tunamwamini Bwana mmoja Yesu Kristo, Mwana wa pekee wa Mungu, aliyezaliwa na Baba kabla ya enzi zote, Mungu kutoka kwa Mungu, Nuru kutoka kwa Nuru, Mungu wa Kweli kutoka kwa Mungu wa Kweli, aliyezaliwa ambaye hakuumbwa, wa asili sawa na Baba, Ambaye kwa ajili yetu sisi wanadamu na kwa wokovu wetu alishuka kutoka mbinguni na kufanywa mwili na Roho Mtakatifu na Bikira Maria na akawa binadamu. (Mt. 1:20-23; Yn. 1:14; 6:38; Lk. 19:10) Ambaye kwa ajili yetu pia, alisulubishwa chini ya Pontio Pilato, aliteseka na akazikwa. (Mt. 27:1-2; Mk. 15:24-39, 43-47; Mdo. 13:29; Rum. 5:8; Ebr. 2:10; 13:12) Siku ya tatu akafufuka, kama yanenavyo maandiko; (Mk. 16:5-7; Lk. 24:6-8; Mdo 1:3; Rum. 6:9; 10:9; 2 Tim. 2:8) alipaa mbinguni, na ameketi mkono wa kuume wa Baba. (Mk. 16:19; Efe. 1:19-20) Atakuja tena katika utukufu kuwahukumu walio hai na waliokufa, na Ufalme wake hautakuwa na mwisho. (Isa. 9:7; Mt. 24:30; Yn. 5:22; Mdo. 1:11; 17:31; Rum. 14:9; 2 Kor. 5:10; 2 Tim. 4:1) (Yn. 1:1-2; 3:18; 8:58; 14:9-10; 20:28; Kol. 1:15, 17; Ebr. 1:3-6) ambaye kupitia yeye vitu vyote viliumbwa. (Yn. 1:3; Kol. 1:16) Tunamwamini Roho Mtakatifu, Bwana na mpaji wa uzima, ( Mwa. 1:1-2; Ayu. 33:4; Zab. 104:30; 139.7-8; Lk. 4:18-19; Yoh. 3:5-6; Mdo 1.1-2; 1 Kor. 2:11; Ufu. 3:22) atokaye kwa Baba na Mwana, (Yn. 14:16-18, 26; 15:26; 20:22) ambaye pamoja na Baba na Mwana anaabudiwa na kutukuzwa; (Isa. 6:3; Mt. 28:19; 2 Kor. 13:14; Ufu. 4:8) Ambaye alinena kwa njia ya manabii. (Hes. 11:29; Mik. 3:8; Mdo. 2:17-18; 2 Pet. 1:21)
Tunaamini katika Kanisa moja takatifu, la ulimwengu mzima na la kitume. (Mt. 16:18; Efe. 5:25-28; 1 Kor. 1:2; 10:17; 1 Tim. 3:15; Ufu. 7:9)
Tunautambua ubatizo mmoja kwa ondoleo la dhambi (Mdo. 22:16; 1 Pet. 3:21; Efe. 4:4-5) Na tunatazamia ufufuo wa wafu na uzima wa wakati ujao. (Isa. 11:6-10; Mik. 4:1-7; Lk. 18:29-30; Ufu. 21:1-5; 21:22-22:5) Amina.
Made with FlippingBook Digital Publishing Software