https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi
9 6 /
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
4. Huu ni usimulizi wa kwanza wa Injili na muhtasari wa hadithi: ulimwengu uko vitani, na Mungu ndiye Shujaa wa vita.
E. Madokezo kuhusu utendaji wa Mungu kama Shujaa wa kiungu katika Agano la Kale
1. Katika nyakati za kabla ya utawala wa kifalme, Mungu anaonekana kama Shujaa anayeshinda bahari au mto (Kut. 15:4-10; Amu. 5:19 21; Zab. 68:22-23; Hab. 3:8-15).
a. Bahari ni ishara ya machafuko na vurugu, inayotazamwa katika mtazamo wa hali isiyo na utulivu, ya machafuko, au hata ya kutisha.
2
b. Mungu anapomshinda adui huyu, uumbaji unarudi kwenye uhai wake na kutoa mazao mengi, Kumb. 23:28; Zab. 68:10-11.
2. Mungu ni Shujaa, aliyemshinda Farao na majeshi yake walipojaribu kuwaangamiza watu wake wa agano, Israeli, Kut. 15:3-4.
3. Zaburi zinamzungumzia Mungu wa Israeli kama Mungu anayeheshimu utawala wake, na atainua mfalme wake wa ukoo wa Daudi kwa nguvu na ulinzi (k.m., Zab. 2; 18; 24; 46; 48; 76; 89; 97; 132; 144).
4. Manabii walimtaja Yehova Mungu kuwa ni Bwana mkuu ambaye aliongoza majeshi yake vitani kwa ajili ya watu wake na heshima yake (Isa. 6; Mika 1:2-4; Sef. 1:14-18; Yoeli 2:1-11).
Made with FlippingBook Annual report maker