https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi
/ 9 5
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
2. Chanzo cha uasi wake kilikuwa ni wivu dhidi ya Mungu kama matokeo ya kiburi, Isa. 14:12-15.
3. Uzuri na utukufu wake wa ajabu ulimfanya aasi mamlaka ya Mungu, Eze. 28:12-18.
4. Uasi huu wa kiroho ndio mzizi na sababu ya aina nyingine zote za uasi miongoni mwa wanadamu leo, 1 Yoh. 5:19.
C. Anguko kama ushiriki wa wanadamu katika uasi wa enzi: kiburi, tamaa, na uchoyo (ubinafsi), Mwa. 3:1-7.
2
1. Majaribu na kutotii: Hawa na nyoka, 2 Kor. 11:2.
2. Kupoteza uhuru: kuingia kwa dhambi na utumwa wa shetani.
3. Kupotea kwa uzima na ukamilifu: mwanzo wa magonjwa na uhalisia wa kifo.
4. Mwisho wa haki: kuvunjika na kugawanyika kwa mahusiano ya kibinadamu.
D. Protoevangelium : tangazo la kwanza la Injili, Mwa. 3:15.
1. Mungu ataweka uadui kati ya uzao wa nyoka na Uzao wa mwanamke.
2. Uzao wa mwanamke utaponda kichwa cha nyoka.
3. Nyoka atauponda kisigino Uzao wa mwanamke.
Made with FlippingBook Annual report maker