https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi

/ 9 7

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

5. Kama matokeo ya kutotii na uasi wa Israeli dhidi ya Mungu, Bwana kupitia hukumu yake na utumwa wa Israeli na Yuda akawa Shujaa aliyepigana dhidi ya watu wake mwenyewe.

a. Yereremia 12:7

b. Yeremia 15:14

c. Maombolezo 2:3-5

2

6. Manabii wa Israeli walipokuwa wakiendelea kupokea ufunuo juu ya ujio wa Masihi, walimtaja Mungu kama Shujaa wa kiungu ambaye angezikabili mamlaka zinazokuja kama ilivyonenwa katika mashairi ya kale zaidi ya Israeli kuhusu Shujaa wa kiungu (k.m., Isa. 26:16 27:6; 59:15b-20; 63:1-6; Zek. 9:1-17; 14:1-21).

F. Ahadi ya mwana wa Daudi: Mfalme atakaye tawala kwa haki.

1. Mungu alitoa ahadi nzito kupitia kwa manabii kwamba atarejesha utawala wake katikati ya watu wake na duniani, Isa. 9:6-7.

2. Mataifa yangeitikia ubwana wake wa haki na amani, Zab. 72:8-11.

3. Mfalme huyu wa Israeli, ambaye angerudisha utawala wa haki wa Mungu, angekuwa wa nyumba ya Daudi, 2 Sam. 7:8-.

4. Mataifa ya dunia yangemsujudia mtawala huyu aliyeinuliwa ambaye Mungu alimtawaza katika mamlaka yake, Zab. 2; Zab. 110.

Made with FlippingBook Annual report maker