https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi
/ 1 0 1
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
C. Utume ni tangazo kwamba Ufalme umekuja katika Bwana Yesu Kristo. Katika Yesu Kristo, Ufalme upo tayari, lakini bado haujakamilishwa .
1. Mitume walihubiri katika ujumbe wao wa utume kwamba Yesu wa Nazareti, ambaye alisulubiwa, ndiye Masihi (Mdo. 2:32-36).
2. Yesu alijielewa kama utimilifu wa unabii wa Kimasihi kuhusu Mtumishi wa Mungu anayeteseka (Luka 24:26-27, 44-48).
3. Yesu aliyekataliwa na viongozi na taifa la Israeli amepandishwa cheo na kuwa Jiwe Kuu la Pembeni (Mdo. 4:11-12).
2
4. Yesu amepewa mamlaka yote na Mungu, na anatangazwa kuwa Bwana wa wote aliyeinuliwa (Mt. 28:18).
a. Matendo 5:30-31
b. Matendo 10:36 – Neno lile alilowapelekea wana wa Israeli akihubiri habari njema ya amani kwa Yesu Kristo (ndiye Bwana wa wote).
5. Kiini cha ujumbe wa mitume walipokuwa wakisafiri na kuhubiri Habari Njema kilikuwa kwamba Yesu ndiye utimilifu wa unabii wa Kimasihi na kwamba utawala wa ufalme wake sasa upo (Mdo. 28:23, 31).
6. Utawala wa Yesu unatambuliwa katika historia ya Kanisa.
a. Christus Victum : Yesu kama dhabihu kuu kwa ajili ya dhambi.
Made with FlippingBook Annual report maker