https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi
1 0 2 /
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
b. Christus Victor : Yesu kama Bwana mshindi juu ya maadui wa Mungu.
c. Christus Vicar : Yesu kama aliyeinuliwa kuwa Kichwa cha Kanisa lake.
Ufalme wa Mungu unamaanisha ushindi wa Mungu juu ya adui zake, ushindi ambao unapaswa kutimizwa katika hatua tatu; na ushindi wa kwanza umekwisha tokea. Nguvu za Ufalme wa Mungu zimevamia milki ya Shetani – Enzi hii ya sasa ya uovu. Shughuli ya nguvu hii ya kuwakomboa wanadamu kutoka katika utawala wa kishetani ilithibitishwa katika kutoa pepo. Kwa hiyo, Shetani alifungwa; alitupwa chini kutoka katika nafasi yake ya mamlaka; nguvu zake “ziliharibiwa.” Baraka za Enzi ya Kimasihi sasa zinapatikana kwa wale wanaoukubali Ufalme wa Mungu. Ni kweli kwamba tayari tunafurahia baraka zinazotokana na kushindwa huku kwa kwanza kwa Shetani. Hii haimaanishi kwamba tunafurahia utimilifu wa baraka za Mungu, au kwamba yote ambayo Ufalme wa Mungu unahusisha yamekuja kwetu.... Ujio wa Pili wa Kristo ni muhimu kabisa kwa utimilifu na ukamilifu wa kazi ya ukombozi ya Mungu. Hata hivyo, Mungu tayari amekamilisha hatua kuu ya kwanza katika kazi Yake ya ukombozi. Shetani ndiye mungu wa Enzi hii, lakini nguvu za Shetani zimevunjwa ili wanadamu wapate fursa ya kuupokea utawala wa Mungu maishani mwao. ~ George Ladd. The Gospel of the Kingdom . Grand Rapids: Wm. B. Eerdmans Publishing Company, 1999. uk. 50.
2
III. Utawala wa Mungu unavamia Enzi hii ya uovu ya sasa kupitia wanajeshi wa Kanisa
A. Uwepo wenye nguvu wa Roho Mtakatifu wa Mungu. Efe. 5:18 – Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho.
1. Roho ndiye ishara ya uwepo na uhakika wa Ufalme, 2 Kor. 1:21-22.
Made with FlippingBook Annual report maker