https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi

/ 1 0 3

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

2. Waamini wote katika Kristo wametiwa muhuri na Roho kama ahadi ya urithi wa siku zijazo (yaani, arabuni au “malipo ya awali” ya udhihirisho kamili la Ufalme ujao, Efe. 1:13; 4:30).

B. Kanisa kama Ishara na Kionjo cha Ufalme, Efe. 5:25-32.

1. Kuwekwa kama mashahidi wake mpaka miisho ya dunia, Mdo. 1:8.

2. Mabalozi wa Kristo na Ufalme wake, 2 Kor. 5:18-21.

2

3. Udhihirisho wa utukufu wa Mungu wa eskatolojia, 1 Pet. 2:9-10.

4. Manaibu wa mamlaka ya Kristo, Mt. 28:18-20; 16:18-19.

C. Kusudi la Mungu katika enzi hii ya sasa: kuwezesha na kuidhinisha Kanisa lake kufanya vita dhidi ya maadui zake, kutoa ushuhuda wa utawala wa Mungu leo.

1. Mamlaka ya Yesu sasa ni kamili mbinguni na duniani: Baba amempandisha kwenye cheo cha Bwana wa wote, taz. Mt. 28:18 pamoja na Flp. 2:9-11.

2. Mtu mwenye nguvu lazima afungwe: Mamlaka ya Yesu juu ya Shetani lazima yatekelezwe (hata kama Shetani amekwisha kushindwa), 1 Pet. 5:8 pamoja na Yak. 4:7.

3. Kanisa ni naibu na wakala wa Ufalme wa Mungu: limepewa haki na mamlaka ya kuwakilisha mamlaka ya Kristo duniani, kufanya vurugu dhidi ya mamlaka na vyombo vyote vinavyopinga ujuzi na mamlaka ya Mungu, 2 Kor. 10:3-5.

Made with FlippingBook Annual report maker