https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi

/ 1 3 7

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

1. Sodoma na Gomora zilipatwa na ghadhabu na hukumu ya Mungu kwa sababu ya uasherati na uonevu wake usiozuilika, Kum. 32:32-33; Eze. 16:49-50; taz. Mwa. 19:24-29.

2. Yeriko iliharibiwa na Mungu katika vita alivyovifanya dhidi ya Kanaani, na laana ikatamkwa juu ya wale ambao wangejaribu kuichukua tena ili kuijenga upya misingi na malango yake (ikiashiria hitaji la watu kukataa kabisa jaribio lolote la kuwasha upya moto wa ibada ya sanamu na uasi dhidi ya Mungu).

a. Yosh. 6:26

b. 1 Fal. 16:34

3

3. Israeli wanapojenga miji yao wenyewe, miji yao pia inaangukiwa katika aina zile zile za mitazamo na tabia zinazohusishwa na wale waliojenga miji kwa kumdharau Mungu.

a. Ibrahimu na mababa wa taifa la Israeli walikuwa wageni, wakiishi katika mahema, bila kujenga miji, Ebr. 11:9-10.

b. Inaonekana wazi kwamba kulikuwa na uhusiano kati ya kutegemea usalama wa mji na kuacha au kukataa usalama wa Bwana: Rehoboamu. (1) 2 Nya. 11:5-12 (2) 2 Nya. 12:1 – Utawala wa Rehoboamu ulipoimarishwa, naye akawa na nguvu, aliiacha sheria ya Bwana, na Israeli wote pamoja naye.

c. Manabii walihubiri daima dhidi ya mwelekeo wa kutegemea majiji yenye kuta kwa ajili ya msaada badala ya Mungu. (1) Zab. 9:6-9

Made with FlippingBook Annual report maker