https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi

1 4 2 /

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

Hitimisho

» Dhana ya mji wa kale inazaliwa kutokana na uhusiano wake na kujitegemea, kiburi, na uasi dhidi ya Mungu. Katika kesi baada ya kesi kuanzia na Ninawi hadi Yerusalemu, Mungu amehukumu miji kwa sababu ya uovu na makosa yao. » Kupitia uchaguzi wake wa dhana ya mji, kwa neema na ukuu wake, Mungu ameikubali dhana ya mji na kuihusisha na uwepo wake mwenyewe, kuugeuza mji kuwa mahali pa makimbilio, toba, na urejesho. Tafadhali chukua muda mwingi uwezavyo kujibu maswali haya na mengine ambayo yametokana na video. Katika sehemu hii tuliona chimbuko na maendeleo ya dhana ya mji. Mji wa kale uliozaliwa katika uasi na kiburi cha Kaini, ulitungwa kiroho katika uhusiano wa kina wa kujitegemea, kiburi, na uasi dhidi ya Mungu. Katika visa vingi, Mungu alihukumu miji kwa sababu ya ibada ya sanamu, ukosefu wa haki, na uovu. Hata hivyo, kwa rehema na upendo wa Mungu, alilichagua wazo la mji na kulifanya la kwake mwenyewe, akiligeuza kuwa makao yake mwenyewe, na kulifanya upya kuwa mahali pa kimbilio, toba, na urejesho. Kama kiongozi wa Kikristo wa mjini, unapaswa kuelewa dhana hizi vizuri, na, inapofaa, utumie Maandiko kuthibitisha majibu yako. 1. Toa muhtasari wa baadhi ya sifa za jumla za miji ya kale. Kwa mtazamo wa kibiblia, dhana hiyo ilianzia wapi? Miji ya kale ilitofautishwaje na vijiji? 2. Kwa nini uhusiano wa uanzishwaji wa miji na Kaini ni wazo muhimu sana la kiroho? Tunaweza kujifunza nini kutokana na tukio la Mnara wa Babeli kuhusu asili ya mji huo? Vivyo hivyo, mji wa Babeli unatusaidiaje kuelewa kuhusu hali ya kiroho ya kutomcha Mungu inayotawala mijini kwa ujumla? 3. Ni miji gani inayotajwa katika Biblia ambayo ilipata hukumu ya Mungu kwa sababu ya dhambi na ukosefu wao wa toba? Kwa nini Yerusalemu ilishutumiwa hasa kwa kujidhania kwa uongo kwamba ina usalama na uwezo? 4. Ingawa miji ilihusianishwa na uasi wa wanadamu, Mungu alikubalije dhana ya mji kama taswira ya makao yake na baraka zake? Je, mfano wa Sayuni (Yerusalemu) unadhihirishaje uteuzi huu wa neema na ukuu wa Mungu? Mungu ameamua nini hasa kuhusu Yerusalemu kuhusiana na uwepo na utukufu wake mwenyewe?

Sehemu ya 1

Maswali kwa Wanafunzi na Majibu

3

Made with FlippingBook Annual report maker