https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi

/ 1 4 3

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

5. Eleza asili ya “ajabu ya kimungu” inayohusishwa na Mungu, picha ya kidunia ya mji, na namna Mungu alivyoibadilisha kuwa taswira mpya na tofauti. 6. Namna gani kitendo cha Mungu kutenga miji sita ya makimbilio, na msamaha wake kwa Ninawi, vinabadili kabisa maoni yetu juu ya mji wa kidunia ambao inaonekana kwamba hauwezi tena kukombolewa? Eleza. 7. Ni kitu gani kinatupatia uhakika kwamba, kwa jiji lolote linalotubu, Mungu anaweza kuwatazama wakaaji wake na kuwapa rehema yake, hata pale wanapokabiliwa na hukumu na kifo? 8. Soma uchambuzi wa Ryken hapa chini wa wajibu wetu wa Kikristo kwa kuzingatia kitendo cha Mungu kubadilisha taswira ya mji kutoka kituo cha uasi hadi mahali pa uwepo wake. Je, unafikiri nini juu ya maoni ya mwandishi huyu kuhusu jinsi tunavyopaswa kutenda sasa kwa kuzingatia taswira hii ya mji iliyobadilishwa na Mungu? Kwa kuzingatia tafsiri zinazounda taswira ya mji, maisha ya Kikristo yanapaswa kuonyesha sifa fulani. Kwanza, Mkristo ni raia wa mji wa Mungu kwa njia ya haki inayopatikana kwa imani, si kwa matendo ya sheria. Kwa mfano, Paulo analinganisha mitazamo hii miwili na “Yerusalemu ya juu” na “Yerusalemu ya sasa” (Gal. 4:22-26; taz. Flp. 3:20). Watu wanaojaribu wenyewe kujihesabia haki mbele za Mungu ni raia wa Yerusalemu hii ya pili, wakati wale wanaomtazamia Kristo kwa imani ni raia wa ile ya kwanza. Pili, maisha ya Kikristo yanatambulika kwa kuwa na heshima kwa serikali ya kibinadamu kama chombo cha muda cha Mungu kwa ajili ya utaratibu tangu Anguko na kabla ya utimilifu (Mt. 22:21; Rum. 13:1-7; 1 Pet. 2:13-17); kwa hiyo, mwamini anapaswa kuishi kama Yusufu au Danieli kuhusiana na ulimwengu unaomzunguka. Waraka wa kale wa Diognetus, utetezi wa Ukristo, unawaelezea Wakristo kama “wanaoishi katika nchi zao, lakini kama wapitaji tu; wanabeba sehemu yao ya majukumu yote kama raia, na wanavumilia magumu yote kama wageni. Kila nchi ya kigeni ni nchi yao, na kila nchi ni nchi ya kigeni.... Wapo katika dunia, lakini uraia wao uko mbinguni” (Waraka kwa Diognetus 5:1-9). Je! Mabadiliko aliyoyaleta Mungu juu ya dhana ya mji yanapaswa kuathirije maisha yetu leo?

3

Made with FlippingBook Annual report maker