https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi

1 4 4 /

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

Tatu, maisha ya imani yamekusudiwa kuwa maisha ya uhakika katika ahadi ya Mungu ya kuanzisha mji wake. Waebrania inazungumza juu ya imani ambayo kwayo Ibrahimu “alikaa ugenini katika ile nchi ya ahadi, kama katika nchi isiyo yake, akikaa katika hema…. Maana alikuwa akiutazamia mji wenye misingi, ambao mwenye kuubuni na kuujenga ni Mungu” (Ebr 11:9-10). Uraia wa mbinguni unapaswa kuwa msingi wa imani katika majaribu ya maisha, na lengo ambalo kwalo maisha yanaelekezwa. Lakini tofauti kubwa inawatofautisha waamini wa Agano Jipya na wenzao wa A.K. Kuhusu hao wa mwisho tunaambiwa, “Hawa wote wakafa katika imani, wasijazipokea zile ahadi, bali wakaziona tokea mbali na kuzishangilia….” (Ebr. 11:13). Wakati Mkristo anapaswa kuendelea katika hali hii ya ugeni hadi utimilifu (1 Pet. 1.1; 2:11), kwa maana ya kina sana na ya kweli upitaji umeisha kwa sababu ya kazi ya upatanisho ya Kristo (Efe. 2:19). Kupitia uaminifu wa kudumu wa Yesu (Ebr. 12:2), Wakristo wameufikia “mlima Sayuni, na mji wa Mungu aliye hai, Yerusalemu wa mbinguni…” (Ebr. 12:22). Kwa hiyo wakati udhihirisho wa kijiografia wa jiji la Mungu bado ni ujao, umeanzishwa milele mbinguni kupitia kazi ya Yesu, na waaminio katika Yesu tayari wamechukua makazi huko (Yoh. 14:1-3) kupitia kuunganishwa naye (Efe. 2:6). Kwa hiyo Kanisa la Yesu linaishi ulimwenguni sasa kama “mji mtakatifu wa Mungu uliowekwa juu ya mlima” (Mt. 5:14). Augustine alieleza hivyo. “Mji mnyenyekevu ni jamii ya watu watakatifu na malaika wema; mji wa kiburi ni jamii ya watu waovu na malaika waovu. Mji mmoja ulianza na upendo wa Mungu; mwingine ulikuwa na mwanzo wake katika upendo wa kibinafsi” (Mji wa Mungu 14:13). ~Leland Ryken. The Dictionary of Biblical Imagery. (kielektroniki). Downers Grove, IL: InterVarsity Press, 2000. uk. 153-154.

3

Made with FlippingBook Annual report maker