https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi
/ 1 4 5
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
Utume wa Kikristo na Jiji Sehemu ya 2: Sababu Muhimu za Utume Mjini
Mchungaji Dkt. Don L. Davis
Kuna sababu tatu muhimu zinazo thibitisha vya kutosha kwa nini utume wa mijini lazima uwe kipaumbele cha shughuli zote za utume leo: mji ni makao ya ushawishi, nguvu, na shughuli za kiroho duniani, unazidi kuwa sumaku inayowavutia waliokandamizwa, waliovunjika moyo, na maskini, na mji unaonekana kama picha ya hatima na urithi wetu wa kiroho. Miji ilikuwa na sehemu muhimu katika huduma ya Yesu na mitume. Huduma ya Yesu mwenyewe ya kutangaza ufalme ilijikita katika miji, na agizo lake la kutangaza Injili lilihusu kuanzia Yerusalemu. Zaidi ya hayo, Ukristo ulizaliwa katika mji, na kuenea katika himaya ya Kirumi katika karne ya kwanza kupitia miji mikuu ya wakati huo (katika maeneo kama vile Dameski, Antiokia, Korintho, Filipi, Thesalonike, Athene, na Roma yenyewe). Shida na fursa nyingi zile zile zinazohusiana na miji ya nyakati za Yesu na siku za mitume zipo hata leo kwa wakazi wa mijini. Majiji ya kisasa ya ulimwengu ni mengi kwa ukubwa, upeo, na idadi ya watu, nayo yanatumika kuwa vitovu vya kitaifa na vya ulimwengu vya serikali, elimu, afya, habari, burudani, biashara, uchumi, viwanda, sheria, jeshi, na dini. Miji inajulikana leo kwa utambulisho na mwelekeo wake, iwe ni miji ya kitamaduni, kisiasa na kiutawala, ya viwanda, ya kibiashara, ya ishara au ya msingi. Miji ya ulimwengu wa sasa inatumika kama sumaku kwa waliokandamizwa, waliovunjika moyo, na maskini. Biblia inafunua ushuhuda ulio wazi na wenye nguvu kuhusu moyo wa Mungu kwa maskini, na ikiwa Mungu anawajali maskini, yeye vilevile anajishughulisha na majiji ya Marekani na dunia kwa sababu ya idadi kubwa ya watu wa tabaka la chini na familia maskini zinazoishi kwa kujazana humo. Mji ni picha na ishara ya hatima na urithi wetu wa kiroho, Yerusalemu Mpya, ambapo Mungu atakaa na Kristo ataabudiwa. Lengo la wazi la utume ni kuvuna miji ya dunia ili kujaza Yerusalemu Mpya, mama wa kweli wa waamini wote (mradi wa mwisho wa ukarabati wa miji). Kwa sababu ya umaana wa mji katika Maandiko na katika ulimwengu wa sasa, miji lazima isalie kuwa kitovu cha shughuli zote za kimishenari. Lengo letu katika sehemu hii, Sababu Muhimu za Utume Mjini , ni kukuwezesha kuona kwamba: • Kuna sababu tatu muhimu zinazo thibitisha vya kutosha kwa nini utume wa mijini lazima uwe kipaumbele cha shughuli zote za utume leo: mji ni makao ya ushawishi, nguvu, na shughuli za kiroho duniani, unazidi kuwa
Muhtasari wa Sehemu ya 2
3
Made with FlippingBook Annual report maker