https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi
1 4 6 /
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
sumaku inayowavutia waliokandamizwa, waliovunjika moyo, na maskini, na mji unaonekana kama picha ya hatima na urithi wetu wa kiroho. • Miji ilikuwa na sehemu muhimu katika huduma ya Yesu na mitume. Huduma ya Yesu mwenyewe ya kutangaza ufalme ilijikita katika jiji, na agizo lake la kutangaza Injili lilihusu kuanzia Yerusalemu. Zaidi ya hayo, Ukristo ulizaliwa katika mji, na kuenea katika himaya ya Kirumi katika karne ya kwanza kupitia miji mikuu ya wakati huo (katika maeneo kama vile Dameski, Antiokia, Korintho, Filipi, Thesalonike, Athene, na Roma yenyewe). • Huduma ya mitume baada ya Kristo ilikuwa imejikita katika kuifikia miji ya ufalme wa Kirumi, kuanzia Yerusalemu, kuelekea Samaria na Yudea, hadi pembe za mbali sana za ufalme wa Kirumi. Safari za Paulo kama zilivyorekodiwa katika Matendo ya Mitume kwa hakika zilikuwa za mijini kabisa, zikitokea katika vituo vilivyothibitika kuwa lango la ufalme mpana wa Kirumi. • Shida nyingi na fursa zinazohusiana na miji ya nyakati za Yesu na siku za mitume pia zipo kwa wakazi wa mijini wa leo. Majiji ya ulimwengu wa sasa ni mengi kwa ukubwa, upeo, na idadi ya watu, nayo hutumika kuwa vitovu vya kitaifa na vya ulimwengu vya serikali, elimu, afya, habari, burudani, biashara, uchumi, viwanda, sheria, jeshi, na dini. • Wanaanthropolojia huainisha miji kulingana na utambulisho na mwelekeo wake. Kuna miji ya kitamaduni (ambayo inaongoza ulimwengu kwa mitindo, mienendo na mawazo), miji ya kisiasa na kiutawala (vituo vya vyombo vya maamuzi ulimwenguni kote, au vituo vya mamlaka za kiserikali na urasimu wake), miji ya viwanda (miji yenye kelele na shughuli nyingi za uzalishaji wa viwandani) miji ya kibiashara (masoko na maduka makubwa ambapo bidhaa na huduma hubadilishwa kwa kiwango cha kimataifa), miji ya alama au ya kihistoria (miji ambayo mapambano makubwa ya kihistoria yanapiganwa, kutatuliwa, na kuwekewa alama za kumbukumbu), na miji ya msingi (ambayo inachanganya sifa zote pamoja). • Miji ya ulimwengu wa sasa inatumika kama sumaku kwa waliokandamizwa, waliovunjika moyo, na maskini. Biblia inafunua ushuhuda wa wazi na wenye nguvu kuhusu moyo wa Mungu kwa maskini, na mwelekeo wa ukuaji wa miji (na mlundikano wa makundi ya watu maskini ndani yake) kama sifa kuu ya hali ya miji ya nyakati za sasa. Hoja hiyo ni ya kimantiki na ya wazi: ikiwa Mungu anawajali maskini, yeye vilevile anajishughulisha
3
Made with FlippingBook Annual report maker