https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi
/ 1 4 7
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
na majiji ya Marekani na dunia kwa sababu ya idadi kubwa ya watu wa tabaka la chini na familia maskini zinazoishi kwa kujazana humo. • Biblia inaonyesha wazi jinsi mji ulivyo picha na ishara ya hatima na urithi wetu wa kiroho. Tumaini la watakatifu ni kukaa na Mungu katika Yerusalemu Mpya, si mahali ambapo Mungu hayupo na ambapo majivuno yanatawala, bali ni nyumba ya wenye haki ambapo Mungu yupo, na Yesu anaabudiwa kama Bwana wa wote. • Lengo la wazi la utume ni kuvuna miji ya dunia ili kujaza Yerusalemu Mpya, mama wa kweli wa waamini wote (mradi wa mwisho wa ukarabati wa miji). • Kwa sababu ya umuhimu wa mji katika Maandiko na katika ulimwengu wa sasa, mji lazima ubaki kuwa kitovu cha shughuli zote za kimishenari. Kuomba kwetu, kutoa, na kutuma watenda kazi lazima kulenge kufikia miji ambayo haijafikiwa, lazima tuajiri wamishenari zaidi kuhudumu katika mji, kupanga mikakati ya jinsi ya kufikia miji ambayo haijafikiwa na Injili, na kuombea miji na kutafuta usalama wake, yaani kutafuta usalama wetu katika uhifadhi wake. Mathayo 9:35-38 – Naye Yesu alikuwa akizunguka katika miji yote na vijiji, akifundisha katika masinagogi yao, na kuihubiri habari njema ya ufalme, na kuponya magonjwa yote na udhaifu wa kila aina. 36 Na alipowaona makutano, aliwahurumia, kwa sababu walikuwa wamechoka na kutawanyika kama kondoo wasio na mchungaji. 37 Ndipo alipowaambia wanafunzi wake, Mavuno ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache. 38 Basi mwombeni Bwana wa mavuno, apeleke watenda kazi katika mavuno yake. Utume unafanya kile ambacho Yesu alifanya. Yesu alikwenda mahali ambapo watu walikuwa, na popote watu walipo utapata haja ya kimkakati ya kuonyesha mwanga na nguvu ya Ufalme wa Mungu.
3
I. Jiji ni kitovu cha ushawishi, nguvu, na shughuli za kiroho
Muhtasari wa Sehemu ya 2 ya Video
A. Yesu na mitume walitekeleza huduma yao ya ufalme kupitia huduma ya kuzunguka mijini.
Made with FlippingBook Annual report maker