https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi
3 0 /
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
C. Picha nne za utume katika Maandiko
Theolojia kwanza ni shughuli ya kufikiri na kuzungumza juu ya Mungu (kufanya theolojia), na pili ni zao la shughuli hiyo (theolojia ya Luther, au ya Wesley, au ya Finney, au ya Wimber, au Packer, au ya yeyote yule). Kama shughuli, theolojia ni shina la taaluma zinazohusiana ingawa tofauti: kufafanua maandiko (eksejesia au ufafanuzi), kuunganisha kile wanachosema juu ya mambo wanayoshughulikia (theolojia ya kibiblia), kuona jinsi imani ilivyoelezewa zamani (theolojia ya kihistoria), kuyapangilia kwa ajili ya matumizi ya leo (theolojia ya utaratibu), kutafuta athari zake kwa mwenendo (maadili) kuyathibitisha na kuyatetea kama kweli na hekima (utetezi), kufafanua kazi ya Kikristo ulimwenguni (misiolojia), kuhifadhi maarifa na nyenzo kwa ajili ya maisha katika Kristo (kiroho) na ibada ya ushirika (liturujia), na kupata elimu ya huduma (theolojia ya vitendo). ~J. I. Packer, Concise Theology: A Guide to Historic Christian Beliefs. (toleo la kielektroniki. Wheaton,
1. Utume ni Tamthilia ya Nyakati Zote : Mungu ndiye mhusika mkuu katika hadithi kuu ya nyakati zote.
2. Utume ni utimilifu wa ahadi ya Mungu : ni utendaji wa Mungu akitimiza ahadi yake kama Mungu mwaminifu kwa agano lake.
1
3. Utume ni Mapenzi ya Enzi : Mungu kama Bwana-arusi wa jamii yake mpya ya wanadamu waliokombolewa.
4. Utume ni Vita vya Milki : Mungu kama Shujaa akianzisha tena utawala wake juu ya ulimwengu.
II. Utume kama Tamthilia ya Nyakati Zote
Tangu Kabla ya Wakati hadi Baada ya Wakati. Imechukuliwa kutoka kwa Suzanne de Dietrich, God’s Unfolding Purpose (Philadelphia: Westminster Press, 1976).
A. Kabla ya Wakati (Umilele Uliopita), Zab. 90:1-2 – Wewe, Bwana, umekuwa makao yetu, Kizazi baada ya kizazi. 2 Kabla haijazaliwa milima, wala hujaiumba dunia, Na tangu milele hata milele ndiwe Mungu.
1. Mungu wa Utatu wa milele, Zab. 102:24-27.
2. Kusudi la Mungu la milele, 2 Tim. 1:9; Isa. 14:26-27.
a. Kulitukuza jina lake katika uumbaji, Mit. 16:4; Zab. 135:6; Isa. 48:11.
IL: Tyndale House Publishers, 1995 .
Made with FlippingBook Annual report maker