https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi

/ 3 9

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

Tafadhali chukua muda mwingi uwezavyo kujibu maswali haya na mengine ambayo yametokana na video. Katika sehemu hii tulitoa « prolegomena » au «neno la kwanza» kuhusu mfumo wa umisheni wa kibiblia, ikijumuisha ufafanuzi wake kama tangazo la fursa ya wokovu na ukombozi wa Mungu kwa njia ya Yesu Kristo na kazi yake, katika uwezo wa Roho Mtakatifu kwa makundi yote ya watu . Ukitazamwa kama tamthilia na hadithi ya Mungu, tangu Kabla ya Wakati hadi Baada ya Wakati , tunaweza kuanza kuona katika hadithi ya utume jinsi Mungu wa Utatu anavyotenda kazi kama Mungu Mwenyezi, akitenda kazi katika mambo yote kwa utukufu wake na manufaa yetu. Tutakachotafuta kutimiza katika somo hili ni «picha kuu» ambayo ni msingi wa asili ya utume katika Maandiko, na hatua ya kwanza ni kuelewa mada zinazozungumzwa katika sehemu hii. Pitia mawazo makuu ya sehemu hii kwa kujibu kwa umakini maswali yaliyo hapa chini, na uthibitishe majibu yako kwa kutumia Maandiko. 1. Nini maana ya neno “ prolegomena ,” na kwa nini tunahitaji “ prolegomena juu ya utume” ambayo inaanza na mtazamo wa kibiblia kuhusu Mungu na kazi yake ulimwenguni katika Yesu wa Nazareti? 2. Fafanua neno “utume,” na uorodheshe vipengele muhimu vinavyoelezea ufahamu wa kibiblia wa utume. Kwa nini ni muhimu sana kwamba mtazamo wetu wa umisheni uanze na Maandiko yenyewe, na si kwa uzoefu wa wamishenari na mashirika ya kimisheni katika historia yote? 3. Kwa nini mtazamo wa kibiblia wa utume, pia, lazima ujengwe katika Yesu Kristo na kazi yake, na kuchukua kwa umakini jinsi Biblia inavyojadili utume kwa namna ya kuzingatia taswira, picha, na hadithi? 4. Je, taswira au picha kuu nne za kitheolojia za utume ambazo zinaweza kupatikana katika Maandiko ni zipi, na kila moja ina fasili (maana) gani? 5. Orodhesha vipengele vikuu vya taswira ya Tamthilia ya Nyakati Zote , na hasa awamu ya Kabla ya Wakati , Mwanzo wa Wakati , na Kufunuliwa kwa Wakati . Angazia vipengele vikuu vya kila awamu moja, na ueleze umuhimu wa kila awamu katika kuelewa umisheni. 6. Eleza kusudi la Mungu linaloendelea kujifunua katika awamu za Utimilifu wa Wakati , Nyakati za Mwisho , Ukamilifu wa Wakati , na Baada ya Wakati za utume kama taswira ya Tamthilia ya `Nyakati Zote . Tena, onyesha mambo makuu ya kila moja ya awamu hizi, na ueleze jukumu na uhusiano wa awamu husika na dhana ya utume wa ulimwengu.

Sehemu ya 1

Maswali kwa Wanafunzi na Majibu

1

Made with FlippingBook Annual report maker