https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi

4 0 /

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

7. Je, taswira ya umisheni kama Tamthilia ya Nyakati Zote inaelezeaje kusudi na jukumu kuu la Mungu katika awamu zinazoendelea kujifunua za tamthilia ya kimungu? Je, taswira hii inatuwezeshaje kuona utume kama urejeshaji wa kile kilichopotea mwanzoni mwa wakati, na kufanya wanafunzi kama kutimiza jukumu letu mahususi katika tamthilia takatifu ya Mungu?

1

Misiolojia ni elimu rasmi ya utume wa Kanisa. Misiolojia ni elimu iliyopangiliwa ya umisheni wa kanisa la Kristo. Kwa hiyo ni taaluma ndani ya theolojia, inayojumuisha mikondo kadhaa. Masomo ya Biblia yanachunguza msingi wa utume wa kanisa katika missio Dei, wito wa Israeli kuwa nuru kwa mataifa yote (Isa. 49:6), na agizo la Yesu kwa wanafunzi wake kuwa mashahidi wake hadi miisho ya nchi na mwisho wa nyakati (Mt. 28:18-20; Mdo 1:8). Eliumu ya kihistoria inachunguza ukuaji na upanuzi wa kanisa katika vipindi mbalimbali na kutathmini athari zake kwa jamii na tamaduni tofauti. Theolojia ya utaratibu inachunguza mwingiliano wa imani ya Kikristo na falsafa na itikadi za kilimwengu na mifumo mingine ya imani. Masomo ya kimaadili, yanajumuishwa katika misiolojia ambapo kanisa lina wajibu wa kutangaza mapenzi ya Mungu kwa ajili ya maisha kwa ujumla wake.... Theolojia ya kichungaji inatafuta njia za kuwafundisha waongofu wapya na kuwajumuisha katika kanisa. Kwa sababu ya wigo wake mpana, misiolojia ina jukumu muhimu katika ujumuishaji wa maeneo mengine ya kitheolojia. Kwa maneno mengine, kila kipengele cha theolojia kina mwelekeo usioepukika wa misiolojia, kwa kuwa kila kipengele kimoja kipo kwa ajili ya utume wa kanisa.

~ J. A. Kirk. “Missiology.” The New Dictionary of Theology . S. B. Ferguson, mh. (toleo la kielektroniki). Downers Grove, IL: InterVarsity Press, 2000. uk. 434.

Made with FlippingBook Annual report maker