https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi
/ 4 1
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
Maono na Msingi wa Kibiblia wa Utume wa Kikristo: Sehemu ya Kwanza Sehemu ya 2: Utume kama Utimilifu wa ahadi ya Mungu
Mchungaji Dkt. Don L. Davis
Taswira ya Utume kama Utimilifu wa ahadi ya Mungu inaelezea kazi ya Mungu kama kutimiza ahadi yake kama Mungu mwaminifu kwa agano lake kwa Ibrahimu na Daudi. Ikijengwa juu ya jukumu la agano la kibiblia katika Maandiko, mada hii inaanza na ahadi ya Mungu ya agano kwa Ibrahimu, iliyothibitishwa kwa wanawe na mababa au taifa la Israeli, na baadaye kuhusishwa na kabila la Yuda. Ahadi hiyo ya agano kwa ajili ya Mzao ambaye angekuwa baraka kwamataifa ilikuzwa na kufafanuliwa katika ahadi kwa Daudi ya kuwa na mrithi wa kudumu kwenye kiti chake cha ufalme. Sasa katika wakati huu na katika nafsi ya Yesu wa Nazareti, ahadi ya Mungu kwa Ibrahimu na Daudi imetimizwa. Vivyo hivyo, katika enzi hii kwa njia ya kutangaza Injili kupitia utume, ahadi ya maisha mapya inatolewa kwa mataifa kwa njia ya mahubiri ya Neno la msalaba. Lengo letu katika sehemu hii, Utume kama Utimilifu wa ahadi ya Mungu , ni kukuwezesha kuona kwamba: • Mojawapo ya motifu (mada) kuu nne zinazoelezea utume katika Maandiko ni motifu ya utume kama utimilifu wa ahadi ya Mungu . Kwa maana ya kibiblia, agano ni mapatano au mkataba kati ya pande mbili, iwe watu binafsi, makabila, au mataifa; pamoja na kuwa na wajibu wa kutimiza masharti ya mkataba huo, na faida na manufaa kama matokeo ya kutimizwa kwa masharti hayo. • Maagano ya Kibiblia ni mengi, na yana sifa zinazofanana, ikijumuisha jinsi maagano na/au mikataba ilivyosimamiwa na shahidi na kubeba madhara makubwa endapo wahusika wangevunja masharti ya maagano au mikataba hiyo (kuvunja mkataba kulichukuliwa kuwa ni uovu mkubwa sana kimaadili). Maagano yalitiwa muhuri na kutolewa ushahidi kwa kutoa zawadi, kula chakula, na mara nyingi yalijumuisha kuweka mawe ya ukumbusho. Yalithibitishwa kwa kula kiapo na kutoa dhabihu. • Pengine aina ya kawaida ya agano la kibiblia ilikuwa sherehe ya ndoa, na maagano mengine maarufu yanaweza kuonekana katika historia yote ya Israeli, kwa mfano, agano la Mungu na Nuhu, na agano lake na wana wa Israeli Sinai. Maagano ya Mungu, yawe yenye masharti au yasiyo na
Muhtasari wa Sehemu ya 2
1
Made with FlippingBook Annual report maker