https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi

4 2 /

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

masharti, yote yanazungumzia mkataba mzito kati ya Mungu na watu binafsi au na watu wake wateule. • Taswira ya utume kama utimilifu wa ahadi ya Mungu inaweza kufuatiliwa kutoka agano la Mungu alilofanya na Ibrahimu, pamoja na sharti lake la kwamba aondoke katika nchi yake na jamaa yake na kwenda katika nchi aliyoichagua Mungu mwenyewe, pamoja na baraka inayoambatana na sharti hilo kwamba Mungu angemfanya kuwa taifa kubwa, angembariki na kulikuza jina lake, kuwabariki wambarikio na kuwalaani wamlaanio, na kuzibariki jamaa zote za dunia kupitia yeye. • Agano la Mungu na Abrahamu la kumleta Mzao ambaye angekuwa baraka kwa mataifa lilihuishwa na kuthibitishwa katika wazao wa Abrahamu, Isaka na Yakobo, na baadaye likafafanuliwa kwa ajili ya Yuda, kabila ambalo Masihi wa Mungu angetokea. Miongoni mwa familia za Yuda, nyumba ya Daudi ilichaguliwa na Mungu kuwa nyumba ambayo Uzao wa kifalme wa baraka za Abrahamu ungetokea. Mrithi wa Daudi angetawala milele juu ya nyumba ya Israeli na kuwa baraka kwa mataifa. • Ahadi ya Mungu kwa Ibrahimu na Daudi ilitimizwa katika nafsi ya Yesu wa Nazareti, ambaye anawakilisha Mzao wa Abrahamu na mwana wa Daudi ambaye kupitia yeye utawala wa Mungu ungesimamishwa. Kupitia maisha, kifo, ufufuo, na kupaa kwa Yesu, ahadi ya agano la Mungu inatimizwa. • Utume ni uthibitisho na utangazaji wa Habari Njema hii kuhusu uaminifu wa agano la Mungu kupia Yesu Kristo, na Agizo Kuu ni jukumu la kutangaza na kufundisha ahadi hii iliyotimizwa kwa ajili ya wanadamu wote, kuanzia Yerusalemu, hadi miisho kabisa ya dunia. • Kiini cha kazi ya umishenari ni kwamba kupitia Yesu wa Nazareti, ahadi ya Mungu kwa Ibrahimu na Daudi imetimizwa na sasa, kwa njia ya kutangaza Injili, ahadi ya uzima wa milele inatolewa bure kwa mataifa kwa njia ya kuhubiriwa kwa Neno la msalaba.

1

Made with FlippingBook Annual report maker