https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi

/ 4 3

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

Ahadi katika Biblia

Katika Agano la Kale la Kiebrania hakuna neno maalum kwa dhana au tendo la kuahidi. Wakati ambapo tafsiri zetu za Kiingereza husema kwamba mtu fulani aliahidi jambo fulani, Kiebrania kinasema tu kwamba mtu fulani alisema au alitamka ( ‘amar, dabar ) neno fulani linalorejelea tendo la wakati ujao. Katika Agano Jipya neno la kitaalamu, epangelia , linaonekana hasa katika Matendo, Wagalatia, Warumi na Waebrania. Ahadi ni neno linaloenda mbele katika wakati ujao. Linatangulia mbele ya msemaji wake na mpokeaji wake, ili kuashiria miadi au makubaliano kati yao kuhusu siku zijazo. Ahadi inaweza kuwa hakikisho la tendo endelevu au la tendo la siku zijazo kwa niaba ya mtu: “Nitakuwa pamoja nawe”, “Wale wanaoomboleza watafarijiwa”, “Tukiziungama dhambi zetu, Mungu atatusamehe dhambi zetu.” Inaweza kuwa makubaliano ya dhati ya uhusiano wa kudumu, ya pande mbili (kama hazilingani): kama ilivyo katika maagano. Huenda ikawa tangazo la tukio la wakati ujao: “Utakapokuwa umekwisha kuwatoa hao watu katika Misri, mtamwabudu Mungu katika mlima huu.” ~ J. W. L Hoad. “Promise.” The New Bible Dictionary . D. R. W. Wood, mh. (toleo la 3, toleo la kiel.). Downers Grove: InterVarsity Press, 1996. uk. 963.

1

I. Utume ni utimilifu wa ahadi ya Mungu: ni utendaji wa Mungu akitimiza ahadi yake kama Mungu mwaminifu kwa agano lake.

Muhtasari wa Sehemu ya 2 ya Video

A. Maana ya agano.

1. Kiebrania, “ brit ,” “kukata.” Neno linalotumika kwa mikataba na shughuli (au miamala) tofauti kati ya Mungu na wanadamu, na kati ya watu.

a. Limetafsiriwa kama “washirika,” Oba. 1:7 BHN.

b. Neno tunalotumia kama “Agano” la Kale na Jipya lina maana sawa na “mkataba.”

2. Linaweza kuzungumzia mkataba kati ya pande mbili, iwe watu binafsi, makabila, au mataifa.

Made with FlippingBook Annual report maker