https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi
/ 4 5
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
a. Hilo lilifunga mkataba kati ya pande hizo mbili.
b. Lilionyesha kielelezo kwa macho kile ambacho kingetokea ikiwa wahusika wangekiuka tamko lao la ahadi.
B. Mifano ya maagano ya kibiblia kati ya Mungu na wengine.
1. Agano na Nuhu ( kwamba hukumu ya mvua isingetokea tena, na kwamba majira na mzunguko wa mchana na usiku havitakoma ), Mwa. 9:8-13.
1
2. Agano la Sinai na wana wa Israeli ( kutolewa kwa Amri Kumi na Sheria kupitia Musa, ili kupokea thawabu ya mafanikio kwa kuzishika Amri na Sheria, na hukumu kwa kutotii ).
a. Kut. 24:3
b. Kut. 34:28
c. Kumb. 4:13
d. Kumb. 29:1
II. Utume ni utimilifu wa ahadi ya Mungu: ni utendaji wa Mungu akitimiza ahadi yake kama Mungu mwaminifu kwa agano lake.
A. Kutolewa kwa Ahadi – Agano na Ibrahimu: tumaini la Uzao.
Made with FlippingBook Annual report maker