https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi
4 6 /
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
1. Hali ya agano na baraka nne, Mwa. 12:1-3.
a. Sharti: Toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonyesha (Mwa. 12:1).
b. Baraka (1) Nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa. (2) Nitakubariki na kulikuza jina lako. (3) Nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani. (4) Katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa.
1
2. Ahadi ilihuishwa kwa Ibrahimu, pamoja na ahadi ya mwana na urithi wa watu wengi mno wasioweza kuhesabika, Mwa. 15:4-6.
3. Miaka kumi na minne baada ya agano kufanyika lilisisitizwa tena, na kuthibitishwa kwa mabadiliko ya jina la Abramu kuwa Ibrahimu na kuanzishwa kwa tohara kama ishara ya kukubali agano, Mwa. 17:1-10.
4. Ilithibitishwa baada ya kujaribiwa kwa moyo wa Ibrahimu kupitia kumtoa Isaka kama dhabihu kwa amri ya Mungu, Mwa. 22:16-18.
B. Kuthibitishwa kwa Ahadi kwa Mababa
1. Ilithibitishwa kwa Isaka, Mwa. 26:24-25.
2. Ilithibitishwa kwa Yakobo, Mwa. 28:13-14.
Made with FlippingBook Annual report maker