https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi

/ 4 9

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

d. Yer. 33:15-18

Yesu kama Kiini cha Ahadi Kati ya Agano la Kale na Agano Jipya

e. Dan. 7:13-14

Kiini cha muunganiko wa ahadi za Agano la Kale (kwa Ibrahimu, Musa, Daudi na Mababa kupitia manabii) ni Yesu Kristo. Ahadi

4. Mataifa wangeshiriki katika kukamilishwa kwa ahadi ya Mungu kwa Daudi, Mdo. 15:15-18 (rej. Amosi 9:11-12).

zote za Mungu zimethibitishwa ndani yake, na kupitia kwake

E. Kutimizwa kwa Ahadi: katika nafsi ya Yesu wa Nazareti, ahadi ya Mungu kwa Ibrahimu na Daudi imetimizwa.

1

zinathibitishwa na kanisa katika tamko la ‘Amina’ la ibada yake (2 Kor. 1:20). Nukuu za Agano la Kale na madokezo katika simulizi za Injili yanaonyesha utimilifu huu. Magnificat [wimbo wa Mariamu alipokutana na Elizabeti] na Benedictus [wimbo wa kuhani Zakaria siku ya tohara ya mwanawe] zinafurahia kwamba Mungu ametimiza neno lake. Neno lililoahidiwa limekuwa mwili. Agano jipya limezinduliwa—juu ya ‘ahadi zilizo bora zaidi’ zilizotabiriwa na Yeremia (Yer. 31; Ebr. 8:6-13). Yesu ndiye mdhamini wake (Ebr. 7:22), na Roho Mtakatifu wa ahadi ndiye arabuni yake (Efe. 1:13-14). ~ J. W. L Hoad. “Promise.” The New Bible Dictionary. D. R. W. Wood, mh. (toleo la 3, toleo la kiel.). Downers Grove: InterVarsity Press, 1996. uk. 963.

1. Kabla ya kuzaliwa kwake, ahadi kuhusu uhusiano wa Yesu na Daudi kama Mzao wa kifalme ulioahidiwa ilifafanuliwa, Luka 1:32-33.

2. Agano kwa Ibrahimu kwa hakika ni ujumbe wa Injili aliopewa Ibrahimu; Yesu ndiye Mzao anayezungumzwa katika agano la Mungu kwa Ibrahimu, Gal. 3:16.

3. Ahadi za kutawala juu ya Ufalme zilitolewa kwa Masihi Yesu.

a. Ebr. 1:8 (taz. Zab. 45:4-6)

b. Rum. 14:8-9

4. Kuvunjwa kwa mwili wa Yesu na kumwagwa kwa damu yake juu ya msalaba kumezindua agano jipya na wale wanaoamini, kwa Wayahudi na watu wa mataifa, na kuleta msamaha na uzima wa milele.

Made with FlippingBook Annual report maker