https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi
/ 8 3
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
3. Wayahudi walikuwa wakimtarajia Masihi ambaye angewakomboa watu wa Mungu Israeli, taz. Yoh. 4:22, Isa. 12:6; 46:13; Sef. 3:16; Zek. 9:9.
4. Ufafanuzi wa Kanisa
a. Ekklesia - (Kiy. “Kuita kutoka”) mara 111 katika Agano Jipya. (1) “Kusanyiko,” taz. Mdo 19:39, 7:38 (2) “Walioitwa,” taz. Rum. 8:30; 1 Kor. 1:2, 2 Kor. 6:17
2
b. Kuriakon - (Kiy. “Yaliyo ya Bwana”) (1) “Karamu ya Bwana,” 1 Kor. 11:20 (2) “Siku ya Bwana,” Ufu. 1:10
C. Riwaya ya Kiyahudi ya mapenzi?: Masihi Yesu kama bwana-arusi na sasa, Kanisa kama bibi-arusi wake!
1. Masihi Yesu ndiye bwana-arusi (Yohana Mbatizaji ndiye rafiki wa bwana-arusi!), Yoh. 3:29.
2. Ufalme wa mbinguni ni kama mfalme anayemwandalia mwanawe karamu ya arusi (lakini hakuna aliyealikwa aliyejitokeza kuhudhuria), Mt. 22:1-14.
a. Wengi walialikwa lakini walijawa na visingizio.
b. Ili kuijaza karamu, watumwa waliagizwa kwenda kualika watu wengine, wakaja kwa furaha (Mataifa?).
Made with FlippingBook Annual report maker