https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi
/ 8 5
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
3. Nukuu ya Wakolosai: Kristo kati ya Mataifa, tumaini la utukufu , Kol. 1:24-29.
E. Injili sasa inatangazwa kwa Mataifa, ambao pamoja na Wayahudi, wamekuwa sehemu ya jamii mpya ya watu wa Mungu na bibi-arusi wa Kristo.
1. Wale wanaoamini wamejumuishwa katika ahadi ya Mungu kwa Ibrahimu, Gal. 3:7-9.
2. Mitume kwenye baraza la Yerusalemu walitambua kwamba manabii waliona kwamba Mataifa pia wataliitia Jina la Bwana, Mdo. 15:13-18.
2
3. Watu wa Mataifa ambao walikuwa wageni kwa ahadi ya Mungu sasa wamejumuishwa ndani ya watu wa agano la Mungu kwa imani katika damu ya Kristo Yesu, Efe. 2:12-13, Rum. 9:24-26.
4. Kiini hasa cha huduma ya kitume sasa ni kuwatayarisha watu wa Mungu (pamoja na Mataifa) kama bibi-arusi wa Bwana Yesu, 2 Kor. 11:2.
5. Kristo anawatayarisha watu wake, Wayahudi na Mataifa, kuwa bibi arusi wake wakati wa kutokea kwake, Efe. 5:25-27.
a. Anamtakasa bibi-arusi wake kwa Neno la kweli (Yoh. 17:17-19; Mdo 26:18; 1 Kor. 6:11; Tito 2:14).
b. Sisi tulioamini, Wayahudi na Mataifa, tutaletwa tukiwa watakatifu pasipo mawaa mbele zake, 2 Kor. 4:14; Kol. 1:22; 2 Kor. 11:2; Yuda 1:24.
Made with FlippingBook Annual report maker