https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi
8 6 /
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
F. Kukamilishwa kwa Mapenzi: Yerusalemu Mpya, Mji wa Mungu, Ufu. 21:1-4.
Uhusiano wa Mawazo na Ufunuo
Dhana ya Kikristo ya kibiblia ya mawazo itatofautisha kati ya kuwaza kwa msingi wa makosa ya kimtazamo, kwa msingi wa picha au taswira, na kuwaza kama ufunuo wa neno la kweli. Shughuli ya ubunifu ya binadamu ni tofauti kabisa na hisia au kufikiri kwa kawaida, lakini pia ni shughuli ya kweli inayohusiana na utendaji kazi wote wa binadamu. Kuwaza ni zawadi ya Mungu ambayo kwayo wanadamu huweza kuamini mambo. Kwa uwezo wa kuwaza mtu hujiaminisha na kutenda “kana kwamba hiki… ni kile…” (k.m. Mungu ni mwamba, Isa. 17:10; Kristo ni bwana-arusi, Mt. 25:1 13). Mawazo ya mwanadamu ndio chanzo cha maarifa ya sitiari na ucheshi ambavyo ni muhimu sana kwa mtindo wa maisha wa mtu yeyote. Kuwaza kunakusudiwa kuwa wakati wa msingi, muhimu, wa faida katika kila kitu wanachofanya watoto wa kuasili wa Mungu. Kuwaza kunakuwa laana tu ikiwa kunafanyika katika ubatili. ~ C. Seerveld. “Imagination.” The New Dictionary of Theology . S. B. Ferguson, mh. (toleo la kielektroniki). Downers Grove: InterVarsity Press, 2000. uk. 331.
2
1. Taswira ya Jiji la Mungu kama bibi-arusi iko wazi, Ufu. 21:2.
2. Ni wale tu waliovalia vazi la arusi ndio watakaoalikwa kuhudhuria, Ufu. 19:7-8.
3. Tutashiriki na Kristo kwa kuwa wamoja naye katika mambo yote, Efe. 5:30-32.
4. Furaha yetu itakuwa kamili, kwa maana muungano huo utakuwa muungano wetu wa milele (utambulisho wetu kamili na bwana-arusi wetu, Masihi Yesu).
Made with FlippingBook Annual report maker