Kristo: Mada Kuu Ya Biblia

Luka: Kristo Anadhihirishwa katika Ubinadamu Wake Mkamilifu Ukoo wa Kristo unafuatiliwa hapa hadi kwa mwanadamu wa kwanza, Adamu. Luka alisisitiza si kile ambacho Yesu alifundisha (kama Mathayo alivyofanya) wali kile alichofanya (kama Marko alivyofanya), bali kile alichotafuta. Luka anaandika, “Kwa maana Mwana wa Adamu alikuja kutafuta na kuokoa kilichopotea” (19:10). Zekaria alitaja mada hii mapema alipoandika, “Tazama, mtu huyu” (6:12). Yohana: Kristo Anadhihirishwa katika Uungu Wake Yohana anaandika, “Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu,” na “Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu” (Yh 1:1, 14). Hafuatilii ukoo wa Kristo hadi ufalme wa kibinadamu (kama Mathayo alivyofanya), japo hauachi bila kujulikana (kama Marko alivyofanya), wala haufuatilii hadi asili ya ubinadamu (kama Luka alivyofanya), bali anaufuatilia hadi kwenye uungu na umilele wake. Katika Yohana, Kristo anaonekana kama tai akipaa mbinguni na, kwa namna tofauti na injili nyingine, katika Injili ya Yohana inadhihirika jinsi Yesu alivyofikiri (taz. Yh 13-17). Katika Mathayo, Yesu anatimiza mahitaji ya mwanadamu kwa habari ya haki (rej. 3:15); katika Marko, hitaji la mwanadamu la huduma (10:45); katika Luka, hitaji la mwanadamu la ukombozi (19:10); na katika Yohana, hitaji la mwanadamu la uzima (10:10). Kwa hiyo, Injili nne zinarekodi udhihirisho wa kihistoria wa Kristo, si kwa ajili ya kikundi fulani cha jamii, wala kwa mabaki fulani ya kidini tu, bali kwa Wayahudi, kwa Wayunani, na kwa Warumi; ndio, kwa ulimwengu wote. Lakini Yesu alikuwa ulimwenguni na “wala ulimwengu haukumtambua. Alikuja kwake, wala walio wake hawakumpokea” (Yh 1:10-11). Ufunuo wa Kristo ulikuwa kwa ajili ya wote, lakini mapokezi ya Kristo yalikuwa kwa wachache walioamini (1:12).

116

Made with FlippingBook Digital Publishing Software