Kristo: Mada Kuu Ya Biblia
MATENDO: UINJILISHAJI AU UENEZAJI HABARI ZA KRISTO Katika Matendo mwelekeo unabadilika kutoka udhihirisho wa kihistoria wa Kristo hadi uinjilishaji wa ulimwengu kwa ujumbe wa Kristo. Yesu alikuwa ameweka mipaka ya huduma yake ya hapa duniani hasa kwa Israeli, lakini alikuwa amewaamuru wanafunzi wake kupeleka ujumbe wake kwa mataifa (Mt. 28:19; Mdo. 1:8). Huko nyuma katika Mwanzo 12, wakati maandalizi yalipofanywa kwa ajili ya Kristo kwa kuchaguliwa kwa Ibrahimu, kusudi lililotajwa na Mungu lilikuwa kwamba “jamaa zote za dunia” zibarikiwe. Utimilifu wa ahadi hiyo umeandikwa katika uenezaji wa ujumbe wa Kristo na mitume katika Matendo. Ufunguo wa Matendo uko katika amri ya Kristo kwa wafuasi wake kuwa mashahidi wake “katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi” (1:8). Kama matokeo ya kumwagwa kwa Roho Mtakatifu, ujumbe wa Kristo uliingia Yerusalemu (sura 1-6); kama matokeo ya mateso makali, injili iliingia Yudea yote (sura ya 7), na Samaria (sura ya 8); na kama tokeo la uongofu wa Paulo na maono ya kimishenari, Kristo alienezwa hadi mwisho wa dunia (sura 9-28, taz. Kol. 1:23). NYARAKA: TAFSIRI NA MATUMIZI YA UJUMBE WA KRISTO Injili na Matendo ya Mitume vinarekodi udhihirisho na uinjilishaji wa Kristo katika ulimwengu wote; Nyaraka za Paulo na za Jumla zinafunua tafsiri na matumizi ya ujumbe wa Kristo kwa waamini. Tofauti hii inasaidia kuelezea kwa nini mbinu ya kufundisha kwa kutumia mifano imeenea sana katika Injili na mbinu ya maelekezo (didactic) inatumika zaidi katika Nyaraka. Kwa kawaida Yesu alizungumza kwa mifano kwa umati ili ukweli ambao haujakubaliwa upate kuwekwa katika maneno ambayo tayari yanakubalika kwao. Nyaraka, kwa upande mwingine, zinazungumza kwa maneno ya moja kwa moja kwa wanafunzi, ambao tayari walikuwa
117
Made with FlippingBook Digital Publishing Software