Kristo: Mada Kuu Ya Biblia

wameikubali kweli lakini walihitaji kufasiriwa zaidi. Kwa hivyo, mbinu ya mifano ilifaa zaidi kwa uinjilishaji na kuifunua kweli kupitia vielelezo, na njia ya maelekezo ya maneno ya moja kwa moja inazaa matunda kwa urahisi zaidi kwa habari ya tafsiri na matumizi ya kweli. Muundo huu wa mwisho ndio unaotumika katika Nyaraka. NYARAKA ZA PAULO: UFAFANUZI KUHUSU KRISTO Mkazo wa msingi katika nyaraka za Paulo ni ufafanuzi au tafsiri ya Kristo kwa waamini, ambayo ilihusisha matumizi ya ufafanuzi huo pia. Katika Nyaraka za Jumla, msisitizo muhimu unahusu mahusia katika mambo ya Kristo au, kwa maneno mengine, matumizi ya ujumbe wa Kristo kwa waamini, ambayo lazima yalihusisha tafsiri kwa namna fulani pia. Paulo kila mara anaweka ufunguo kwenye “mlango wa mbele” wa nyaraka zake, kwa kuwa mada zake kwa ujumla zimeelezwa kama “utajiri” ambao mwamini anao “katika Kristo.” Kwa kawaida, maneno haya yanatokea katika sura ya kwanza ya waraka, na mara nyingi linakuwa rejeo la kwanza la neno “katika Kristo” ambalo hutambulisha mada ya waraka. Utaratibu huu uko wazi kabisa kuanzia katika waraka kwa Warumi hadi 2 Wathesalonike. Warumi: Ukombozi katika Kristo Kitabu hiki ni ufafanuzi mkuu wa “ ukombozi [wa mwamini] ulio katika Kristo Yesu” (3:24). Ni tangazo la haki ya Mungu (1:17), ambayo watu wanahesabiwa kwa njia ya imani katika Yesu Kristo (rej. 4:5). 1 Wakorintho: Utakaso katika Kristo Kitabu hiki kinaelekezwa kwa “wale waliotakaswa katika Kristo Yesu, walioitwa wawe watakatifu” (1:2). Ingawa waraka kwa Warumi unafunua

118

Made with FlippingBook Digital Publishing Software