Kristo: Mada Kuu Ya Biblia

jinsi ambavyo Mungu anaweza kumtangaza mtu kuwa mwenye haki (rej. Rum. 3:21-26), 1 Wakorintho unaonyesha kwamba ni muhimu kumfanya mtu kuwa mwenye haki pia. La kwanza ni tendo la kuhesabiwa haki, na la pili ni mchakato wa kutakaswa. 2 Wakorintho: Shangwe katika Kristo Kwa wale, kama Paulo, wanaojaribu kuishi maisha ya utakaso ambayo yanahusisha hatari na mateso (2 Tim. 3:12, taz. 2Kor. 11:23-), kutakuwa na shangwe (ushindi) katika Kristo. “Ila Mungu ashukuriwe, anayetufanya tushangilie ushindi daima katika Kristo…” (2:14, RSUVDC). Mwamini anapata shangwe ya ushindi katika huduma yake (taz. 1Kor. 4). Wagalatia: Kuwekwa Huru katika Kristo Wagalatia iliandikwa kama onyo juu ya wale “waliingia kwa siri ili kuupeleleza uhuru wetu tulio nao katika Kristo Yesu, ili watutie utumwani” (2:4). Ni tangazo la kuwekwa huru kwa Wakristo. Paulo anawahimiza waamini: “Katika uhuru huo Kristo alituweka huru; kwa hiyo simameni, wala msinaswe tena chini ya kongwa la utumwa” (5:1, RSUVDC). Waefeso: Kuinuliwa na Kuungamanishwa katika Kristo Barua hii inaelekezwa kwa wale waliobarikiwa “katika Kristo kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho ” (1:3). Hata hivyo, kuna mada kadhaa zinazobadilika “katika Kristo.” Mwamini anapokea kuinuliwa huku katika Kristo kwa sababu tu ana uteule katika Kristo (1:4), ambao matokeo yake ni muungano au kuungamanishwa katika Kristo (1:10). Kipengele hiki cha mwisho cha umoja ndicho kinachoonekana kubeba sehemu kubwa ya waraka huu (rej. 2:14; 4:3).

119

Made with FlippingBook Digital Publishing Software