Kristo: Mada Kuu Ya Biblia
Wafilipi: Fahari katika Kristo Kulingana na barua hii, Paulo alitamani kwamba waamini wazidi “kuona fahari katika Kristo Yesu” (1:26). Licha ya ukweli kwamba mtume huyu alikuwa amefungwa, alisema, “nafurahi; tena nafurahi pamoja nanyi nyote. Nanyi vivyo hivyo furahini, tena furahin i pamoja nami” (2:17-18; taz. 1:18). “ Furahini katika Bwana siku zote; tena nasema, Furahini ” (4:4), na, “Hatimaye, ndugu zangu, furahini katika Bwana” (3:1); haya yote ni sehemu ya furaha na fahari ya daima ya Paulo katika Kristo Yesu. Wakolosai: Kukamilika katika Kristo Katika kitabu hiki Paulo anamwonya “kila mtu, na kumfundisha kila mtu katika hekima yote, tupate kumleta kila mtu mtimilifu katika Kristo ” (1:28). Wanaonywa dhidi ya falsafa yoyote ambayo inakana “ utimilifu ” wa uungu wa Kristo (2:9) ili wapate utimilifu wa uzima ndani yake (2:10). Paulo anaomba kwamba wasimame wakiwa “ wakamilifu na kuthibitika sana katika mapenzi yote ya Mungu” (4:12). Hakuna kinachoweza kuongezwa juu ya uungu au huduma ya Kristo, na sisi tumekamilika ndani Yake. 1 Wathesalonike: Matarajio katika Kristo Mtume anaanza barua yake kwa kumshukuru Mungu kwa ajili ya kazi ya Wathesalonike “ya imani, na taabu yenu ya upendo, na saburi yenu ya tumaini lililo katika Bwana wetu Yesu Kristo ” (1:3). Mkazo umewekwa zaidi juu hili la mwisho, kwa kuwa kuja kwa Kristo kunatajwa katika kila sura (1:10; 2:19; 3:13; 4:16; 5:23). Sasa kwa kuwa “tumaini” katika Agano Jipya lina maana ya kuwa na ujasiri katika kile kinachokuja (Ebr. 6:11) na si shauku au matamanio tu, basi ni matarajio katika Kristo ambayo Paulo anaeleza hapa.
120
Made with FlippingBook Digital Publishing Software