Kristo: Mada Kuu Ya Biblia

Filemoni: Wema katika Kristo Kuongoka kwa mtumwa huyu mtoro kunatoa kielelezo bora kabisa cha “kila kitu chema kilicho kwetu, katika Kristo” (mst. 6). Tena, Paulo anasema, “ili kwamba wema wako usiwe kama kwa lazima, bali kwa hiari” (mst. 14). Wema huu au faida hizi katika Kristo zilihusu nyanja ya kimwili, kijamii pamoja na nyanja ya kiroho ya Injili. NYARAKA KWA WATU WOTE: MAHUSIA KATIKA KRISTO Nyaraka za Paulo, hasa zile kumi za kwanza, kwa kiasi kikubwa ni mafafanuzi na tafsiri kuhusu Kristo; Nyaraka za Jumla kimsingi ni matumizi ya ujumbe wa Kristo au mahusia kuhusu Kristo, ingawa zina mafafanuzi pia. Nyaraka hizi pia zinatofautiana na za Paulo kwa kuwa barua zake kwa kawaida zilikuwa za moja kwa moja kwa kanisa fulani au mtu binafsi, wakati Nyaraka za Jumla zililenga hadhira kubwa zaidi (taz. Yak. 1:1; 1Pet. 1:1). Waebrania: Mahusia juu ya Utimilifu Mwandishi aliwahasa Waebrania, akisema, “Kwa sababu hiyo, tukiacha kuyanena mafundisho ya kwanza ya Kristo, tukaze mwendo ili tuufikilie utimilifu ” (6:1). Kristo alikuwa “bora kuliko” kila kitu ambacho Agano la Kale lingeweza kutoa (1:4; 7:19, 22; 8:6, n.k.). Dhabihu za Agano la Kale haziwezi “ kumkamilisha mtu aabuduye” (9:9) lakini Kristo, kupitia “hema iliyo kubwa na kamilifu zaidi” (9:11), na “kwa toleo moja amewakamilisha hata milele hao wanaotakaswa” (10:14). Kwa kuwa Kristo anachukua nafasi ya Agano la Kale, kuna maonyo makali sana kwa wale ambao hawasongi mbele kuufikia ukamilifu katika Kristo (taz. 2:1-4; 10:26; 12:15).

122

Made with FlippingBook Digital Publishing Software