Kristo: Mada Kuu Ya Biblia
Yakobo: Mahusia juu ya Hekima katika Kristo Yakobo anahimiza: “Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima , na aombe dua kwa Mungu,” (1:5). “N’nani aliye na hekima na ufahamu kwenu? Na aonyeshe kazi zake kwa mwenendo wake mzuri, katika upole wa hekima ” (3:13). Kwa hiyo, “matendo” hufuata hekima, na hii “ hekima itokayo juu, kwanza ni safi, tena ni ya amani, ya upole, tayari kusikiliza maneno ya watu, imejaa rehema na matunda mema” (3:17). 1 Petro: Mahusia kuhusu Unyenyekevu Petro anaelekeza barua kwa wale ambao wamepata “kutakaswa na Roho, hata mkapata kutii na kununyiziwa damu ya Yesu Kristo” (1:2). Katika kitabu hiki chote kuna himizo la kunyenyekea (2:13, 18; 5:5) na utii (1:14, 22), na hasa kwa mateso yenye subira. “Lakini kustahimili, mtendapo mema na kupata mateso, huu ndio wema hasa mbele za Mungu” (2:20). 2 Petro: Mahusia juu ya Usafi katika Kristo Kitabu hiki kimeandikiwa “wale waliopata imani.... katika haki ya Mungu wetu, na Mwokozi Yesu Kristo” (1:1), ambaye amewakirimia “vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa , kwa kumjua [Kristo]” (1:3, taz. 3:11). Utauwa na usafi wote huu ni kwa njia ya elimu (“maarifa,” 1:2, 5, 6, 8, n.k.), yaani, kukua “katika neema, na katika kumjua Bwana wetu na Mwokozi Yesu Kristo” (3:18). 1 Yohana: Mahusia kuhusu Ushirika na Kristo Yohana anawahasa waamini: “tukienenda nuruni, kama yeye [Kristo] alivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi” (1:7). Ushirika uko katika nuru (sura 1-2) na katika upendo (sura 3-4), lakini ni pamoja na Mungu na Kristo. “Ushirika wetu ni pamoja na Baba, na pamoja na Mwana wake Yesu Kristo.” (1:3).
123
Made with FlippingBook Digital Publishing Software