Kristo: Mada Kuu Ya Biblia

2 Yohana: Mahusia ya Kuendelea katika Kristo “Nalifurahi mno kwa kuwa nimewaona baadhi ya watoto wako wanaenenda katika kweli” (mst. 4). “Jiangalieni nafsi zenu msiyapoteze mliyoyatenda, bali mpokee thawabu timilifu” (mst. 8). Anazungumza juu ya kudumu (mst. 9) katika kweli, kwa maneno mengine, kuendelea katika Kristo. 3 Yohana: Mahusia kuhusu Michango kwa ajili ya Kristo “Rafiki mpendwa, wewe ni mwaminifu kwa yale unayowatendea ndugu, …. Utafanya vyema ukiwasafirisha [yaani, kulipia gharama za usafiri wao]….. Ilikuwa ni kwa ajili ya hilo Jina waliondoka, bila kukubali kupokea msaada wowote kutoka kwa watu wasioamini. Kwa hiyo imetupasa sisi kuonyesha ukarimu kwa watu kama hao ili tuweze kutenda kazi pamoja kwa ajili ya kweli” (mst. 5-8). Yaani anawasihi watoe mchango kwa ajili ya kazi ya Kristo. Yuda: Ushauri wa Kushindana kwa ajili ya Kristo Yuda anaeleza, “naliona imenilazimu kuwaandikia, ili niwaonye kwamba mwishindanie imani waliyokabidhiwa watakatifu mara moja tu” (mst. 3). Kwa hiyo barua yake fupi ni mahusia ya kuwaweka waamini katika nyanja ya kushindana kwa ajili ya Kristo dhidi ya uasi (taz. 15) kama vile Mikaeli “ aliposhindana na Ibilisi” (mst. 9). Hivyo basi, katika Nyaraka kwa Watu Wote kuna mahusia ya kutendea kazi katika maisha ya mwamini mambo yale ambayo Paulo alitolea ufafanuzi katika nyaraka zake. Nyaraka za Jumla ni matumizi ya kweli ya Kristo kwa waamini, kama ambavyo barua za Paulo zilitoa tafsiri ya Kristo kwa waamini.

124

Made with FlippingBook Digital Publishing Software