Kristo: Mada Kuu Ya Biblia

UFUNUO: MWISHO WA MAMBO YOTE KATIKA KRISTO Sehemu ya mwisho ya Maandiko ni kilele kinachofaa kwa yote yaliyotangulia. Agano la Kale lilimtazamia Kristo kwa matarajio kwa kuwa lilikuwa limeweka msingi kwa ajili yake (Torati), lilifanya matayarisho kwa ajili yake (Historia), lilimtamani kwa shauku (Ushairi), na kumtazamia kwa matarajio (Unabii). Agano Jipya linamtazama Kristo katika utimilifu , kwa kuwa amekuja kwa njia ya udhihirisho katika mwili (Injili), amekuwa kusudi la uinjilishaji kwa ulimwengu (Matendo), mada ya tafsiri na utendaji wa mwamini (Nyaraka), na ndiye ambaye ndani yake vitu vyote vitafikia utimilifu wa mwisho (Ufunuo). Katika Injili, Kristo anaonekana kama Nabii kwa watu wake; katika Matendo na Nyaraka Yeye ni Kuhani kwa watu wake; na katika Ufunuo, Kristo ndiye Mfalme juu ya watu wake. Kwanza lilikuja tendo la kufanyika mwili kwa Kristo (Injili), likafuatiwa na kuinuliwa kwake (Matendo na Nyaraka), na kisha kutukuzwa kwake milele (Ufunuo). Vitu vyote viliumbwa na Kristo (Kol. 1:16), vitu vyote vinajumuishwa ndani yake (1:17), na vitu vyote vitahitimishwa katika Yeye (1:20). Hitimisho kwa waaminio wote katika Kristo litakuwa wokovu (Efe. 1:10). Hitimisho kwa wasioamini wote litakuwa kutiishwa chini ya Kristo (Flp. 2:10). Pengine kuna kosa moja tu lisiloweza kusameheka katika kufasiri kitabu cha Ufunuo na kosa hilo ni kutokukiona katika msingi wa Kristo. Zaidi ya mambo yote yaliyomo, kitabu hiki ni “Ufunuo wa Yesu Kristo” (1:1). Kwanza, ni ufunuo wa nafsi ya Kristo. Kisha, ni ufunuo wa mali ya Kristo, kanisa ambalo amelinunua kwa damu yake mwenyewe (1:5). Mwisho, ni ufunuo wa mpango wa Kristo (sura ya 4-22) wa kuuteka ulimwengu huu. Kinatazama mbele kwenye utimilifu wa mwisho wa historia ya mwanadamu wakati “Ufalme wa dunia umekwisha kuwa ufalme wa Bwana wetu na wa Kristo wake” (11:15) na wakati ambapo “maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu” (21:3).

125

Made with FlippingBook Digital Publishing Software