Kristo: Mada Kuu Ya Biblia
SURA YA 6 | NENO LA MUNGU: NENO-MTU NA NENO-ANDISHI KRISTO NA MAANDIKO kadhalika huitwa “Neno la Mungu.” Maandiko yanaitwa «Neno la Mungu» kinyume na «mapokeo» ya Wayahudi (Mk 7:13). Na katika Yohana 10:35 “neno la Mungu” linatumiwa katika maana sawa na “Maandiko” ya Agano la Kale. Kitabu cha Waebrania kinasema “neno la Mungu li hai, tena lina nguvu” (4:12). Paulo anarejelea “neno la Mungu” lisiloshindwa (Rum. 9:6). Matendo ya Mitume inamtaja Paulo kama mtu aliyetumia muda wake “kufundisha neno la Mungu” (taz. 18:11). Pia kuna baadhi ya vifungu ambamo Biblia inaitwa “neno” (rej. Yh. 17:14, 17; Mt. 13:20) au “neno la kweli” (2 Tim. 2:15). Marejeo katika Ufu. 1:2, 9; 6:9; 20:4 kwa “neno la Mungu” pia yanaweza kumaanisha neno la Mungu lililoandikwa, lakini hili haliko wazi. Katika mistari mingine, Kristo anatajwa kuwa “neno la Mungu” (Ufu. 19:13) au “Neno.” Yohana aliandika hivi katika injili yake: “Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. . .. Naye Neno alifanyika mwili” (Yh 1:1, 14). Katika waraka wake wa kwanza Yohana alisema, “Lile lililokuwako tangu mwanzo, tulilolisikia, tuliloliona kwa macho yetu, tulilolitazama, na mikono yetu ikalipapasa, kwa habari ya Neno la uzima ; 2 na uzima huo ulidhihirika, nasi tumeona, tena twashuhudia…” (1:1-2). Hapa Yohana anamshuhudia Kristo, neno lililo hai la Mungu, kama mistari iliyotangulia ilivyozungumza juu ya neno lililoandikwa la Mungu. Neno la Mungu Lililoandikwa Sifa Zinazofanana Hai 2 Tim. 3:16 Asili ya Kimungu Yh 1:1 Ebr. 1:1 Asili ya Mwanadamu Ebr. 2:14 Rum. 3:2 Upatanishi wa Kiyahudi Ebr. 7:14
127
Made with FlippingBook Digital Publishing Software