Kristo: Mada Kuu Ya Biblia
Itatambulika kwamba Kristo ana asili mbili, kadhalika na Maandiko. Kristo ni Mungu na Mwanadamu katika asili yake, na Biblia ni ya kimungu na ya kibinadamu katika asili yake. Yaani, Biblia kwa hakika ni Neno la Mungu lakini pia kwa hakika ni maneno ya wanadamu. Zaidi ya hayo, kama ambavyo Kristo hana dhambi, ndivyo pia Maandiko yanaaminika kuwa hayana makosa. Kristo habadiliki, na Maandiko pia hayabadiliki, na kama ambavyo Kristo alitolewa kwa ulimwengu kupitia taifa la Wayahudi ndivyo ilivyo kwa Maandiko pia. UKUU WA NENO HAI JUU YA NENO LILILOANDIKWA Kwa nini kuna uwiano huu wa karibu kati ya Mwokozi na Maandiko Matakatifu? Kwa nini sifa na kazi zao zinafanana? Majibu ya maswali haya yamo katika asili ya “Neno” la Mungu ni nini, na kwa nini Mungu anazo aina hizi mbili za Neno lake. Neno (Kiyunani: logos ) la Mungu limetumika angalau kwa njia tatu katika Agano Jipya: (1) kama neno la mdomo kutoka kwa (au kuhusu) Mungu (rej. Lk 8:21; Mdo 4:31); (2) kama Neno la Mungu lililoandikwa (Yh. 10:35; Ebr. 4:12, nk.); na (3) kama Neno hai la Mungu (Kristo). Katika kila hali, maana ya kawaida iko katika ukweli kwamba ni usemi au tamko la Mungu; lakini njia ya uwasilishaji inatofautiana. Kwa kuwa maneno ya mdomo na maandishi hutofautiana tu katika namna ambayo sauti hutofautiana na ishara, na kwa kuwa asili ya neno la mdomo la Mungu ilibadilishwa hadi kufanyika Neno lililoandikwa, tofauti hapa kimsingi ni kati ya aina mbili za matamko ya kimungu: tamko lililoandikwa na tamko hai. .
129
Made with FlippingBook Digital Publishing Software