Kristo: Mada Kuu Ya Biblia
Neno la Mungu—Tamko la Kiungu Katika:
Lugha ya Kibinadamu (2 Tim. 3:16)
Maisha ya Kibinadamu (1 Yh 1:1)
Ishara Kauli Kitabu
Mwana ( Ebr. 1:2 )
Mtu (Yh 14:7)
Mwili ( Ebr. 10:5-7 ) Maisha ya Mwanadamu ni Bora kuliko Lugha ya Mwanadamu Kutokana na ulinganisho huu tunaweza kuona kwamba Mungu amejieleza Mwenyewe kwa njia mbili za msingi. Kwanza, Amejieleza katika lugha ya kibinadamu. Kilichoandikwa ( grapha ) ni Neno la Mungu (2 Tim. 3:16). Yesu alisema yale yaliyoandikwa yana mamlaka (Mt. 5:18-), na yanazungumza juu yake (Lk 24:44). Daudi alisema, “Roho ya Bwana ilinena ndani yangu, Na neno lake likawa ulimini mwangu” (2 Sam. 23:2). Paulo anazungumza kuhusu “maneno yanayofundishwa kwa hekima ya kibinadamu, bali yanayofundishwa na Roho” (1Kor. 2:13). Yaani Maandiko ni usemi wa mawazo ya Mungu katika lugha ya mwanadamu. Kuna ufunuo mwingine wa Mungu kwa mwanadamu, ambao ni wa tofauti: ni ufunuo wa kimungu si katika lugha ya kibinadamu lakini katika maisha ya kibinadamu. Kwa kuwa wanadamu “wameshiriki damu na mwili, yeye [Kristo] naye vivyo hivyo alishiriki yayo hayo” (Ebr. 2:14). Kama Yohana alivyosema, “Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu” (Yohana 1:14). Kuna ubora fulani katika aina hii ya usemi wa kiungu. Labda Yohana alieleza vizuri zaidi aliposema, “Lile lililokuwako tangu mwanzo, tulilolisikia, tuliloliona kwa macho yetu, tulilolitazama, na mikono yetu ikalipapasa ….Neno la uzima” (1 Yh 1:1). Yaani, Neno lililo hai la Mungu ni usemi kamili zaidi wa Mungu kuliko Neno lililoandikwa, kwani uwepo wa mpendwa ni bora kuliko barua kutoka kwake. Bila shaka, ikiwa mtu huyo hayupo, basi rekodi ya kile anachotamani kuzungumza ndiyo njia bora
130
Made with FlippingBook Digital Publishing Software