Kristo: Mada Kuu Ya Biblia
zaidi ambayo mtu anaweza kutarajia. Kwa hivyo, ufunuo wa Mungu katika Maandiko ni muhimu, lakini ufunuo wa Mungu katika Kristo ni bora zaidi. Mwana ni Bora Kuliko Ishara Zaidi ya hayo, ufunuo wa Mungu katika Maandiko ni mojawapo ya ishara, kwa maana ya kwamba lugha ni mfumo wa ishara. Lakini ishara ni ishara tu au viwakilishi vya ukweli lakini sio ukweli huo. Kwa mfano, ishara ya mti , inayojumuisha herufi tatu, haiwezi kufananishwa kwa njia yoyote na mti mzuri wenye kijani kibichi unaokua katika bustani. Kadhalika, usemi wa kiishara wa Mungu katika Biblia haupaswi kulinganishwa na Mungu Mwenyewe, kwa maana huo utakuwa ni uabudu Biblia (kuabudu Biblia kama mungu). Usemi wa Mungu kwa njia ya Mwanawe ni tofauti na usemi wake kwa njia ya ishara, kwa kuwa ndani ya Kristo, Neno la Mungu, kuna uhusiano kati ya Mungu na usemi wa Mungu. Yohana alisema, “Neno [usemi wa Mungu] alikuwa Mungu” (Yh 1:1). Mwandishi wa Waebrania anatangaza kwamba Mungu “amesema na sisi katika Mwana” (1:2) ambaye “ni mng’ao wa utukufu wake na chapa ya nafsi yake” (1:3). Ufunuo wa Mungu katika Mwana ni bora zaidi kuliko ufunuo wake katika ishara, iwe ni mifano, kama vivuli vya Agano la Kale (ona sura ya 2), au ishara za lugha ya kibinadamu inayotumiwa katika Biblia. Sababu iko wazi vya kutosha: Neno katika ishara halifanani wala kulingana na Mungu (kwa maana hiyo itakuwa ni ibada ya sanamu), ila kwa upande wa Neno Mwana, Yeye anafanishwa na kulinganishwa na Mungu. Katika ufunuo kupitia ishara kuna uwakilishi wa Mungu tu; katika ufunuo kwa njia ya Mwana kuna utambulisho wa Mungu. Kwa maana Yohana alisema kwamba Kristo Neno si usemi wa Mungu tu, bali katika utambulisho huu wa kipekee, Neno ni Mungu.
131
Made with FlippingBook Digital Publishing Software