Kristo: Mada Kuu Ya Biblia

Mtu ni Bora kuliko Kauli Kufafanua ukuu wa Kristo juu ya Maandiko kwa njia nyingine, Maandiko ni ufunuo katika kauli (propositional revelation) , lakini Kristo ni ufunuo binafsi wa Mungu katika mwili (personal revelation) . Bila shaka, kunaweza kuwa na kauli au maelezo kuhusu mtu, na hivyo ndivyo hasa Maandiko yalivyo. Lakini hili linaunga mkono zaidi hoja ya kwamba mtu ambaye maelezo yameandikwa kwa habari yake ni muhimu zaidi kuliko maelezo yenyewe. Yaani, kusudi la Neno lililoandikwa ni kuwasilisha au kutambulisha Nafsi ya Neno lililo hai. Lakini, ikiwa ndivyo, basi ujumbe wa Maandiko (yaani, mtu aitwaye Kristo) ni bora kuliko njia ya kuwasilisha ujumbe huo (yaani, maelezo kuhusu Kristo). Mwili ni Bora kuliko Kitabu Kuna namna nyingine dhahiri zaidi ambayo Neno la Mungu lililo hai ni bora kuliko Neno la Mungu lililoandikwa. Hii imerekodiwa katika Waebrania 10:5-7, “ Kwa hiyo ajapo ulimwenguni.... mwili uliniwekea tayari; Sadaka za kuteketezwa na sadaka za dhambi hukupendezwa nazo; Ndipo niliposema, Tazama, nimekuja (katika gombo la chuo nimeandikiwa) Niyafanye mapenzi yako, Mungu.” Neno lililoandikwa ni ufunuo katika kitabu; Kristo ni ufunuo wa Mungu katika mwili – mwili ambao unaweza kuwa dhabihu kwa ajili ya dhambi. Hakuna kitabu kinachoweza kufanya upatanisho wa dhambi, kama ilivyofanya dhabihu ya “mwili wa Yesu Kristo mara moja tu” (Ebr. 10:10, taz. Rum. 3:25). Si wino bali ni damu ambayo ilihitajika kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu (Ebr. 9:22). Kitabu kinaweza kutoa ufunuo wa Mungu, lakini ni mwili na damu ya Kristo pekee ndivyo vinavyoweza kuleta upatanisho na Mungu (2 Kor. 5:18-21). Kutokana na tofauti hizi inapaswa kuwekwa dhahiri kwamba ufunuo wa Mungu katika Kristo ni mkuu kuliko ufunuo wake katika Maandiko.

132

Made with FlippingBook Digital Publishing Software